Recent Posts

PropellerAds

Saturday, February 4, 2017

Madini mapya yagunduliwa Mererani, Tanzania

Madini mapya yamegunduliwa nchini
Tanzania, katika eneo lenye madini ya
kipekee la Manyara, na kupewa jina
Merelaniite.
Jina hilo limetokana na eneo ambalo madini
hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika
milima ya Lelatema katika wilaya ya
Simanjiro katika eneo la Manyara.
Eneo hilo linafahamika sana kwa madini ya
Tanzanite.
Madini hayo yaligunduliwa na wataalamu
kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha
Michigan cha Marekani, makavazi ya historia
asilia ya London, chuo kikuu cha Di Firenze
cha Italia na makavazi ya historia asilia ya
Smithsonian ya Washington.
Wataalamu sita waliofanya uchunguzi,
kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida
la Minerals (Madini) wanasema madini hayo
yana vipande vinavyofanana na sharubu vya
rangi ya kijivu vya urefu wa milimita moja
hivi, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa
hadi mililita 12.
Kipenyo cha vipande hivyo ni mikrometa
kadha.
Madini hayo yanakaribiana na madini ya
zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite,
chabazite, tremolite, diopside, quartz, calcite,
graphite, alabandite na wurtzite.
Tanzania kuwaruzuku wachimbaji
wadogo
"Madini haya mapya yametambuliwa na
taasisi inayoyapa majina madini, IMA
CNMNC (2016-042), na kupewa jina
linalotokana na eneo yalipogunduliwa kwa
heshima ya wachimba migodi wa eneo hilo
wa zamani, wanaoishi na wanaofanya kazi,"
makala ya wataalamu hayo inasema.
"Wilaya ya Merelani imekuwa maarufu tangu
mwishoni mwa miaka ya 1960 kutokana na
aina ya madini ya thamani ya rangi ya
samawati kwa jina zoisite yafahamikayo
kama tanzanite, lakini ni eneo muhimu sana
kwa wanaotafuta madini ya kipekee na ni
eneo la kusisimua sana kutafuta madini
mapya," John Jaszczak, mwanafizikia katika
Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Michigan,
na aliyeongoza katika kuandika makala
kuhusu ugunduzi wa madini hayo anasema.
Madini hayo yalitambuliwa mara ya kwanza
mwaka 2012 na Simon Harrison na Michael
Wise, bila wataalamu hao kuyafahamu
vyema, pale walipogundua vitu
vilivyoonekana kama nyaya ndogo zilizokuwa
zimedunga na kuingia ndani ya vipande vya
madini ya chabazite.
Baadaye uchunguzi zaidi ulifanywa na
ikagunduliwa kwamba yalikuwa madini
tofauti.