
Polisi wamesema mwanamume huyo, ambaye ana masharubu yenye kushabihiana na dikteta Hitler, alionekana akijipiga picha nje ya nyumba alimozaliwa dikteta huyo mjini Braunau.
Inaelezwa kuwa kijana huyo alionekana pia katika miji ya Vienna na Graz.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Austria amesema kwamba vitendo vya kijana huyo havikuwa vya masihara hata kidogo ama sanaa ya maonesho, anajua fika alichokuwa akikifanya.