
Mjusi huyu aliyetambuliwa, ni bingwa wa usanii, wanasema wanasayansi, wakiwa na kiwango kikubwa mno cha magamba kuliko aina yoyote ya mjusi duniani.
Ngozi ya mjusi huyo inayofanana na magamba ya samaki, ina mtindo wa kukatika katika.

Aidha, ndani ya magamba hayo kwenye ngozi, kuna maeneo ya kukatika katika.
Hata ingawa jamii nyingi ya mijusi, hawawezi kupoteza ngozi zao kwa urahisi hadi pale wakabwe kwa nguvu, mjusi huyu ana uwezo huo haraka anapoguswa
Ajabu ni kwamba, ngozi na magamba mengine humea kwa kasi sana, kwa kipindi cha wiki chache tu.
Jamii hiyo ya mujusi imegunduliwa katika maeneo ya mapango ya Tsingy, kaskazini mwa Madagascar.