Mwana harakati wa Urusi, Vladimir
Kara Murza, ameondoka nchini baada ya kulazwa hospitali kwa zaidi ya
majuma mawili, akiwa mahututi.
Inashukiwa kuwa mwana harakati huyo alipewa sumu.Karatasi za hospitali zinasema aliugua kutokana na kitu kisichojulikana.
Alisafirishwa kwa ndege kutoka Urusi, akifuatana na mkewe na tabibu, kuenda kuendelea kutibiwa nchi za nje.
Taarifa ilisema kuwa Bwana Kara Murza, ambaye alikuwa mshirika mkubwa wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa, Boris Nemtsov, anakusudia kuendelea na kazi yake ya kurejesha demokrasi nchini Urusi.