Baraza kuu la ushauri linaloongozwa
na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis ,
limechukua hatua isiyokuwa ya kawaida ya kutoa taarifa yenye kuonesha
kuwa linamuunga mkono.
Hali hiyo inafuatia upinzani wa dhahiri
dhidi ya uongozi wa Papa Francis kutoka kwa makundi mbalimbali wakiwemo
makardinali wanne wa kihafidhina ambao kwa uwazi mkubwa walihoji juu ya
misimamo ya papa huyo juu ya talaka kwa wakatoliki.Katika taarifa yake, mshauri mwandamizi wa baraza la ushauri la Makardinali walirejelea tukio la hivi karibuni ingawa hawakufafanua zaidi, wakitilia maanani suala hilo kuwa linamuunga mkono papa na mafundisho yake.