Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameamrisha vikosi
vya kijeshi vipatavyo 440, kutoa usalama katika majengo ya Bunge, wakati
atakapokuwa akilihutubia taifa leo Alhamisi.
Vyama vya upinzani vimelaani hatua hiyo na kusema hiyo ni "kutangaza vita".
Hotuba za hapo awali za Bw Zuma, zilikumbwa na maandamano na fujo, huku wabunge wa upinzani wakitoa wito wa kujiuzulu kwake.
Kwa muongo mmoja uliopita, Bw Zuma amekuwa akiandamwa na madai ya kashfa ya ufisadi.
Taarifa
kutoka kwa Ofisi ya Rais na iliyotolewa siku ya Jumanne, inasema kuwa
Bw Zuma aliamrisha kutumwa kwa vikosi hivyo vya wanajeshi, ili
kushirikiana na maafisa wa polisi kutoa ulinzi.
Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa nchi hiyo, kudumisha usalama, badala ya kuhusika katika sherehe.
Kwa
mjibu wa taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya Habari nchini humo,
duru za kiusalama zimeonya kuwa kutatokea maandamano makubwa katika
hafla hiyo.
Duru hizo zilisababidsha hofu, kwamba huenda polisi wakashindwa kukabiliana nayo.
Hotuba za awali za kitaifa, zilikumbwa na fujo ndani ya Bunge.
Tangu
waliposhinda viti katika uchaguzi mkuu mwaka 2014, wanachama wa chama
cha Economic Freedom Fighters (EFF), wamekuwa wakitatiza hotuba ya Rais
Zuma na vikao vingi vya Bunge kwa kupiga kelele na kumfokea hadharani
Rais kuhusiana na madai hayo ya kashfa ya ufisadi
Mnamo mwaka 2015, wanachama hao wa EFF waliondolewa
katika ukumbi wa Bunge na walinda usalama waliokuwa wakijifanya kama
wahudumu wa Bunge.
Lakini chama kikuu cha upinzani cha Democratic
Alliance (DA) kimelaani vikali hatua hiyo ya Rais, na kueleza kuwa ni
"ya kutamausha mno".
"Matamshi ya mara kwa mara ya Rais Zuma
'kudumisha sheria na usalama' kwenye taarifa yake, kunaashiria matumizi
mabayya ya vikosi vya jeshi nje ya majukumu yao ya kuhusika tu katika
sherehe za kitaifa ndani ya nchi," taaifa ya chama cha DA imesema
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
2 hours ago