Home »
» Mambo yatakayo kufanya ukose heshima kwenye jamii yako
Hakuna
kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu
wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara
makubwa.Ni
imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini
wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu
jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu.Kitaalamu,
hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata
kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na
jinsi tunavyoenenda.Njia
za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya
dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka
maisha ya kudharauliwa.
1. Muonekano.Kwanza
kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi
wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu
anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi
gani.Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi.Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako mbele ya wenzako.
2. Mazungumzo.Hapa
naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au
kukubomolea heshima. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa
kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima
yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi. Biblia inasema penye wingi wa
maneno hapakosi uovu.3. Utendaji wako wa Kazi.Ndugu
zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya
kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba,
jambo hilo halifai kwa vile huchangia kubomoa heshima yako mbele ya
jamii. Fanya kazi usiishi bila kujishughulisha.4. Kutotimiza ahadi.Kama
una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi
unajiweka katika nafasi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii
unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.5. Sifa zisizo na maana.Nakumbuka
msemo mmoja kutoka kwa mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa
falsafa za maisha, marehemu Adolf Balingilaki, ambao unasema kwamba:
“Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei
nafuu.”Msemo
huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya
kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujiinua, watu watakudharau.
6. Kutokuwa mwaminifu.Suala
la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo
kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze kwani ukiwa
mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako