Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, February 1, 2017

Mama atakiwa ''kuthibitisha anatoa maziwa'' uwanja wa ndege

Bi Bose alilazimishwa kuthibitisha iwapo ananyonyesha katika uwanja wa ndege
Mwanamke mmoja amewasilisha malalamishi yake kwa maafisa wa polisi wa Ujerumani akidai kuwa aliambiwa atoe maziwa katika eneo la usalama la uwanja wa ndege ili kuthibitisha kuwa ananyonysha mtoto.
Gayathiri Bose aliambia BBC kwamba alifedheheshwa na hatua hiyo na kuongezea atawasilisha malalamishi yake rasmi mahakamani.
Anasema kuwa maafisa wa polisi katika uwanja wa ndege wa Frankfurt walimtuhumu kwamba alikuwa amebeba pampu ya kutoa maziwa licha ya kwamba hakuwa na mtoto.
Polisi wa Ujerumani wamekataa kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo.Lakini walisema kuwa hatua hiyo sio ya kila siku.
Mtoto wako yuko Wapi?
Bi Bose ambaye alikuwa akisafiri pekee alisema kuwa anaelekea kupanda ndege kuelekea Paris Alhamisi iliopita wakati aliposimamishwa katika sehemu ya kukaguliwa kiusalama.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 33 kutoka Singapore baada ya mkoba wake ambao ulikuwa umebeba pampu hiyo ya maziwa kukaguliwa aliwekwa kando na kuhojiwa.
Je unanyonyesha? Basi mtoto yuko wapi? Mwanao yuko Singapore? Aliulizwa.
Bi Bose alisema kuwa maafisa hao hawakumuamini wakati aliposisitiza kuwa kifaa hicho ni cha kutoa mziwa.
Walichukua paspopti yake na kuizuia na baadaye akapelekwa katika chumba kimoja kwa mahojiano zaidi.
''Ndani ya chumba hicho afisa huyo wa polisi alinitaka kuthibitisha kuwa nanyonyesha na kutoa maziwa'', alisema Bose.
''Na niliwaaambia kwamba hakuna kitu kama hicho, sisi huweka pampu hiyo katika matiti yetu na mashine hufanya kazi hiyo''.
Alitaka nimuonyeshe kwa mkono kupitia kutoa maziwa kidogo.
Bi Bose alisema alikubali na kufinya matiti yake, ''nilikuwa nimeshangazwa na hatua hiyo''.
''Nilikuwa peke yangu na sikujua ni nini kitafanyika iwapo watataka kuniwekea lawama.
Na wakati nilipotoka katika chumba hicho ndipo nilipoelewa kile kilichokuwa kikitendeka.
 Pampu ya maziwa
Nilianza kulia, nilikasirika vibaya''.
Alisema kuwa maafisa waliijaribu pampu hiyo kabla ya kumuachilia huru, kumpatia pasipoti yake apande ndege ya kuelekea Paris.
Bi Bose alichukua jina la afisa huyo na kuliandika katika karatasi.
Bi Bose alisema kuwa kisa hicho ambacho kilifanyika kwa takriban dakika 45 kilikuwa cha kufedhehesha na kushtusha.
''Na waliponiachilia niliwuliza mwajua kwamba hivi sivyo inavyopaswa kumfanyia mtu.Niliwauliza Je ,munajua mulichonifanyia ,mulinifanya kuonyesha titi langu''.
"afisa huyo alisema, umemaliza sasa unaweza kwenda, tafadhali nenda.Afisa huyo hakuwa na huruma wala kuona kwamba ametenda kosa'',aliongezea Bi Bose.