Wanawake wengi bado hawajapata fursa
ya kuchukua nyadhifa za juu katika nchi nyingi, lakini hiyo ni kinyume
kwa Taifa la Caribbean la Turks & Caicos au TCI.
Mwezi Disemba
taifa hilo ambalo ni koloni ya zamani ya Uingereza, lilipata waziri
mkuu wa kwanza mwanamke, Sharlene Cartwright-Robinson. Wanawake pia wanashikilia nyadhifa za naibu gavana, mkuu wa sheria, jaji mkuu, mkuu wa mashtaka na makatibu wengine watano wa kudumu, miongoni mwa nyadhifa zingine.
Kufuatia wanawake kuwalemea wenzao wa kiume, sasa jitihada zinafanywa kuwapa motisha vijana wa ili wajeza kupigania nao nyadhifa za juu.
Waliofanikiwa
Wanawake nchini Turks & Caicos walipataje mafanikio kama hayo ambayo wengi wana ndoto ya kutapata?Bi Cartwright-Robinson ambaye chama chake cha PDM kilipata ushindi mkubwa tarehe 15 kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba anasema kuwa alikuwa "mwanamume bora kwa kazi hiyo"
Akifanya kampeni kwa manifesto ya haki za jamii na serikali yenye uwazi, aliwashinda wagombea wengine 52 kupata wadhifa huo.
Ushindi wake ulifikisha kikomo uongozi wa chama cha PNP wa miaka 13, wa waziri mkuu Michael Misick ambaye anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Anaamini kuwa wanawake hufanya kazi kwa njia inayobora.
"Wanawake huwa waaangalifu zaidi. Tunashikilia nyadhifa ambazo hatujawai na ukweli ni kwamba tunaziendesha kwa njia nzuri," Bi Cartwright-Robinson alisema.
Mwezi Februari mwaka 2014 Bi Braithwaite-Knowles, aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza mkuu wa sheria nchini humo baada ya kufanyika uchaguzi huru kote nchini.
Kwa sasa kati ya wanafunzi 17 kutoka TCI ambao wamepata mafunzo nchi za kigeni 14 ni wanawake.
"Hakuna vizuizi"
Mkuu huyo wa sheria anasema kuwa kile ambacho kitakuwa ni changamoto ni kujaribu kutekeleza majukumu ya kimaisha kama mama kwa mtoto wake wa miaka 7 na mke.Anasema kuwa kwa wanawake kupata nyadhifa kama hizo, wanastahili pongezi. Anasema ni vyema kuonyesha kuwa wamepata nyadhifa hizo kwa njia iliyo ya haki.
Naibu Gavana Williams anakubaliana na hilo.
Wajibu wake ambao ni pili kutoka ule wa London wa John Freeman, pia ulikuwa wazi kwa wagombea kote duniani.
Wajibu wa Bi Williams unahusu kusimamia idara ya wafanyakazi wa umma iliyo na wafanyakazi 1700. Aliapishwa na kujiunga na baraza la mawaziri kwa mara ya pili tarehe 21 mwezi Disemba.
Anaiambia BBC kuwa wanawake wameishikia nyadhifa za juu kwenyr nchi hiyo ya watu 35,000, hasa katika nyanja za elimu, afya, siasa na serikali.