Safari ya ndege kutoka uwanja wa Heathrow hadi San Francisco, ilichelewa kwa saa kadhaa baada ya panya kuonekana ndani ya ndege.
Abiria
waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo ya shirika la Uingereza, walikuwa
tayari wameingia ndani ya ndege hiyo wakati lilitolewa tangazo kuwa
ingechelewa.Carly, ambaye alikuwa ndani ya ndege, alisema kuwa mhudumu alitangaza, "walisema kitu kisicho cha kwaida kimetokea"
Kisha mhudumu huyo akasema wameambiwa ndege nyingine imepatikana lakini abiria wangesubiri saa kadhaa ili kuanza safari.
Kisha safari nyingine ikaanza saa nne baadaye.
Shirika la ndege la Uingereza lilisema; "Tunaelewa kuwa karibu kila mtu anataka kusafiri nasi hadi San Francisco, lakini wakati huu kulikuwa na mteja mdogo ambaye lazima tungemtoa.
"Kila mmoja aliye na miguu miwili kwa sasa yuko safarini kuenda California, na tunaomba radhi kwa kuchelewa."