Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 26, 2017

Mwanamume afa maji huku watu wakimcheka Italia

Mwanamume mmoja raia wa Gambia alikufa
maji huku watu wakitazaka katika eneo la
Venice's Grand Canal nchini Italia.
Gazeti la Times la nchi hiyo linasema kuwa
watu katika mji huo walipiga picha kisa
hicho huku wakicheka na kumtupia maneno
ya ubaguzi wa rangi Pateh Sabally mwenye
umri wa miaka 22.
"Endelea, rudi nyumbani," mmoja wao
aliongea kwa sauti.
Kulingana na shirika la Reuters, majaji nchini
Italia wameanzisha uchunguzi baada ya
video iliyonaswa kwa kutumia simu ya mkoni
siku ya Jumapili kuchapishwa kwenye
mitandao.
Hakuna mtu aliyejaribu kuruka kwenye maji
hayo yenye baridi kumsaidia bwana Sebally,
ambaye anaripotiwa kuwasili nchini Italia
miaka miwli iliyopita.
Lakini vifaa vya kuokoa maisha viliruswa
kwenye maji karibu na mahala alikuwa laniki
hakuonekana kuvifikia, na kuzua uvumi kuwa
alikuwa anataka kujiua.
"Yeye ni mjinga, anataka afe," mtu anasikika
akiongea kwenye video hiyo.
Zaidi ya wahamiaji 181,000 waliwasili Italia
kwa mashua mwaka 2016 wengi kutoka nchi
za Afrika ambalo ni ongezeko la karibu
asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka 2015.