Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 19, 2017

Maporomoko ya theluji yaua 30 hotelini Italia

Waokoaji wanasema kuwa hadi watu 30 wametoweka baada ya hoteli moja katikati mwa Italia kuangukiwa na maporomoko ya theluji yaliosababishwa na tetemeko la ardhi.
Waokoaji walifanya juhudi za usiku kucha kufika katika hoteli ya Rigopiano, huku wa kwanza akifika kwa kutumia ubao wa kutelezea juu ya theleji.

Italia wawaombea waliokufa katika tetemeko la ardhi

Barafu iliosombwa na theluji hiyo ilifunga barabara za kuingia katika eneo hilo.
Mtu mmoja amepatikana amefariki katika barafu hiyo. Wawili wamepatikana wakiwa hai lakini wengine wangi bado wamefukiwa chini ya theluji hiyo.
Afisa mmoja amesema kuwa kuna watu wengi waliofariki katika hoteli hiyo.
Moporomoka ya Theluji yalioangukia Hoteli Rigopiano
Image caption
Moporomoka ya Theluji yalioangukia Hoteli Rigopiano
Eneo la milima katikati mwa Italia lilikabiliwa na msururu wa mitetemeko ya ardhi siku ya Jumatano pamoja na mitetemeko mingine usiku kucha.
Mitetemeko hiyo ya ardhi imesababisha maafa mengi kutokana na kimbunga cha hivi majuzi ambacho kiliangusha miti ya stima mbali na kufunga barabara zinazoelekea vijijini.
Operesheni za uokoaji zinaendelea katika maeneo mengine ya jimbo hilo.

Related Posts:

  • Philadelphia na kodi ya vinywaji Katika mji wa Philadelphia nchini Marekani wameanza kutoza kodi ya vinywaji vyenye sukari na kaboni licha ya kuwepo kwa mamilioni ya kampeni zilizofanywa na kampuni za vinywaji baridi kutaka kufungwa. Meya wa demokrasia ya … Read More
  • HERE ARE THE 100 BEST EDUCATION INFOGRAPHICS “Education is the most powerful weapon which you can use to change the world.”–Nelson Mandela With the world around us ever-changing, education is now more important than ever. Beginning as early as prehistory as a means to… Read More
  • Mkewe Obama amtambua mbunifu kutoka KenyaMkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru. Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjir… Read More
  • TZ yataka uzoefu wa Qatar sekta ya gesiRais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linakusudia kufanya biashara na jamhuri ya Qatar haswa katika sekta ya gesi na usafiri wa ndege. Rais Magufuli aliyasema hayo baada ya kukutana na balozi wa Q… Read More
  • Miaka 90 jela kwa kunajisi wanafunziMwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake. Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaodhulumu wa… Read More