Tanzania inasema kuwa itapokea dola
milioni 305 kama mkopo kutoka kwa Benki
ya Dunia, kugharamia upanuzi wa bandari
kwenye mji wa Dar es Salaam.
Bandari hiyo ndiyo inaunganisha mataifa ya
Afrika ambayo hayapakani na bahari
yakiwemo Zambia, Rwanda, Malawi, Burundi
na Uganda na pia eneo la mashariki mwa
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Benki ya Dunia ilisema katika ripoti ya
mwaka 2014 kwa matatizo kwenye bandari
ya Dar es Salaam yalikuwa yakiigharimu
Tanzania na majirani zake hadi dola milioni
2.6 kila mwaka.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
3 hours ago