Viongozi wa umoja wa Afrika wameamua
kuirudisha Morocco katika shirika la Umoja wa Afrika AU zaidi ya miongo
mitatu baada ya taifa hilo la ufalme wa Afrika Kaskazini kujiondoa
katika AU kufuatia mgogoro wa eneo la Sahara magharibi.
Shirika hilo linatambui Sahara ya Magharibi kuwa jimbo huru, lakini Morrocco inasema kuwa eneo hilo ni mkoa wake wa kusini.- Morocco yataka kujiunga upya na AU
- Mfalme wa Morocco kukutana na Magufuli
- AU kumchagua mwenyekiti mpya wa tume
Eneo la Sahara ya Magharibi linaendelea kuwa eneo tata ,lakini viongozi wengi wa Afrika walipiga kura kuikubali Morrocco kurudi katika Umoja wa Afrika.