Watu 14 wamefukiwa na kifusi katika
mgodi Kaskazini Magharibi mwa Tanzania
walipokuwa wakiendela na shughuli zao za
uchimbaji madini.
Tukio hilo lililotokea leo kwenye mgodi
dhahabu wa RZ katika Kata ya Nyarugusu
mkoani Geita unaomilikiwa na Kampuni ya
China limepelekea watu 14 akiwemo raia
mmoja wa China kufukiwa na kifusi umbali
wa mita 38 (124ft) ardhini.
Zoezi la uokoaji bado zinaendelea na kwa
taarifa za awali ni kuwa mfumo wa
kuingiza hewa ndani ya mgodi huo tayari
imerekebishwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga
alisema kuwa wanaamini kuwa watu hao
watakuwa bado wapo hai na watafanikiwa
kuwaokoa kwa wakati.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
4 hours ago