Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa
wanachama wa al-Shabab wameshambulia
hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia
Mogadishu.
Watu hao wenye silaha wameingia kwenye
hoteli hiyo baada ya kulipuliwa kwa mabomu
mawili kwenye lango la kuingia kwenye hoteli
hiyo.
Kapteni Mohamed Hussein wa kikosi cha
polisi nchini humo ameambia wanahabari
kwamba watu wengi, wakiwemo wanasiasa
walikuwa kwenye hoteli hiyo ya Dayah.
Amesema ufyatulianaji mkali wa risasi bado
unaendelea ndani ya hoteli hiyo.
Idadi kamili ya waliouawa pamoja na
majeruhi haijabainika.