Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 26, 2017

Ajiuzulu baada ya papa kumtaka asambaze kondomu

Kiongozi wa kanisa katoliki anayewasaidia
raia wa Malta amejiuzulu kufuatia mgogoro
na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza
mipira ya kondomu kulingana na kanisa
hilo.
Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67
alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka
kufanya hivyo katika mkutano siku ya
Alhamisi.
hatua hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la
hisani la kanisa hilo huko Malta lilisambaza
maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la
Myanmar.
Kanisa katoliki linakataza utumizi wa mipira
ya kondomu.Papa Francis alimtaka kujiuzulu
na alikubali.
Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama
ule wa taifa zima. Hutoa pasipoti, stampu na
leseni na pia lina uhusiano wa kidiplomasia
na mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.
Ijapokuwa tawi hilo linaonekana kuwa na
wanaume pekee, viongozi wake sio wanaume
pekee.
Kufikia 2013 wanawake walikuwa asilimia 30
wakijulikana kama Dames.
Kundi hilo lilo katika kuondoa sura yake ya
kibwenyenye na kuvutia vipaji ili kuendelea
kazi zake za kibinaadamu.