saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku
kutolewa kwa pesa za serikali ya Marekani
kufadhili mashirika ya nchi za nje ambayo
yanatekeleza au kutoa habari kuhusu utoaji
mimba.
Afisa wake wa mawasiliano Sean Spicer
amesema hatua hiyo ya rais inaonesha
kwamba "anataka kuwatetea Wamarekani
wote, wakiwemo wale ambao hawajazaliwa."
Agizo hilo ambalo kirasmi linafahamika
kama "the Mexico City Policy" (Sera ya Jiji la
Mexico) huenda likayakera makundi ya
kutetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu
uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na
msimamo wake wa kupinga utoaji mimba.
Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba
upigwe marufuku Marekani.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku
dhidi ya ufadhili wa mashirika ya utoaji
mimba nje ya Marekani kutolewa.
Rais wa Republican Ronald Reagan mara ya
kwanza alianzisha Sera ya Jiji la Mexico
mwaka 1984 na kuwa wa kwanza kupiga
marufuku ufadhili huo.
Mambo muhimu kuhusu utawala wa
Trump
Watakaoumia na watakaofaidi chini ya
Trump Marekani
Lakini chama cha Democratic kilibatilisha
marufuku hiyo chini ya utawala wa Bill
Clinton.
Sera hiyo inayataka mashirika yasiyo ya
kiserikali ambayo yanapokea ufadhili wa
serikali ya Marekani kukubali "kutotekeleza
na kutoendeleza au kutohamasisha watu
watumie utoaji mimba kama njia ya uzazi wa
mpango katika nchi nyingine".
Kwa miongo mingi, imekuwa kwamba pesa
za Marekani haziwezi kutumiwa katika utoaji
mimba katika mataifa ya nje.
Lakini Sera ya Jiji la Mexico inaenda hatua
zaidi.
Mwaka 2009, Barack Obama alisitisha
utekelezaji wa sera hiyo, ambayo ilikuwa
imrejeshwa chini ya utawala wa Rais George
Bush.
Makundi ya kutetea uhuru wa wanawake
kuamua kuhusu uzazi wamepinga hatua hiyo
ya Bw Trump.
"Ni jambo la kusikitisha sana kwamba moja
ya hatua za kwanza za Trump inaunganisha
mambo mawili kwa pamoja: kunyamazisha
wote wanaotofautiana naye na
kuwakandamiza wanawake," taarifa kutoka
kwa kundi la Naral Pro-Choice America
imesema.
Trump ayumbayumba kuhusu utoaji
mimba
"Siku mbili baada ya maandamano ya
kihistoria ya wanawake ya kumpinga Trump
kufanyika na siku moja baada ya
maadhimisho ya uamuzi wa kihistoria wa
mahakama kesi ya Roe v. Wade, Donald
Trump anapatia kipaumbele hatua ya
kurejesha ... sera ambayo inawanyamazisha
wahudumu wa afya na kuweka hatarini
wagonjwa."
Wakati wa kampeni, Bw Donald Trump,
ambaye awali alitetea uhuru wa wanawake
kuamua kuhusu uzazi, aliambia MSNBC
kwamba "lazima kuwe na aina fulani ya
adhabu kwa mwanamke" iwapo utoaji mimba
utakuwa marufuku.
Baadaye, aliondoa tamko hilo baada ya
kushutumiwa vikali na makundi ya kutetea
haki za wanawake.
Maafisa wa kampeni wa Bw Trump walisema
waliamini uamuzi kuhusu uhalali wa utoaji
mimba unafaa kuachiwa majimbo yenyewe,
na kwamba adhabu inafaa kutolewa kwa
wanaotoa huduma za utoaji mimba.
Alisema anaunga mkono marufuku ya utoaji
mimba ila tu wakati mimba imetokana na
"ubakaji, kujamiiana kwa maharimu au
wakati maisha ya mama yamo hatarini".
Bw Trump pia ameahidi kujaza nafasi ya jaji
iliyo wazi Mahakama ya Juu na jaji ambaye
ni mhafidhina kuhusu masuala ya kijamii.
Hayo yakijiri, Bunge la Congress limeashiria
nia yake ya kuondoa ufadhili wa serikali kwa
kundi la Planned Parenthood, kundi linalotoa
huduma za afya ya uzazi Marekani na nje ya
taifa hilo.