akiw akatika ziara rasmi nchini
Tanzania leo Jumtatu amesaini
mikataba tisa ya ushirikiano kati ya
nchi hizo mbili.
Rais huyo ametahadharisha nchi za
kiafrika juu ya kuwepo kwa mtandao wa
Fethullah Gulen uliofanya jaribio la
mapinduzi nchini Uturuki mwezi Julai
mwaka jana.
Katika mkutano wa pamoja na Rais John
Magufuli amewaambia waandishi wa
habari umuhimu wa kukuza kiwango
cha biashara baina ya Tanzania na
Uturuki kutoka dola za kimarekani
milioni 150 hivi sasa hadi kufikia dola za
kimarekani milioni 500. Rais Erdogan
aliwasili nchini Jumapili, akiwa katika
ziara ya kikazi ya siku mbili.
Sera ya Uturuki Afrika
Rais Erdogan amesema sera ya uturuki
kuhusu Afrika imejikita katika
kunufaisha pande zote mbili.
Rais huyo aliongeza kusema serikali
yake inafuta njia bora ya kuleta
maendeleo na kuliunganisha bara la
Afrika huku akisema Uturuki kama
mwanachama wa Taasisi ya Kiislam
(OIC) ni ya pili katika nchi zilizo piga
hatua kiuchumi.
Kuhusu mtandao wa Fethullah, rais
huyo wa Uturuki amesema wanachama
wa kiongozi huyo wameenea kila mahali
hivyo ni muhimu kwa nchi mbalimbali
kuchukua tahadhari.
Hata hivyo alisita kuzungumzia uwepo
wa mtandao wa shule zinazodaiwa za
wanachama hao za FEZA zilizopo nchini
humo.
Uongozi wa shule hizo za FEZA nchini
Tanzania katika taarifa maalum wakati
wa vuguvugu la mapinduzi hayo
ilikanusha kuhusika na mtandao huo wa
Fethullah.
Rais John Magufuli
Kwa upande wake mwenyeji wake rais
Magufuli alizungumzia mikakati
mbalimbali ya ukuaji wa uchumi
inayotekelezwa na serikali yake hivi sasa
akigusia maombi ya mkopo kutoka Benki
ya Exim ya Uturuki. Amesema tayari
ameshawasilisha kwenye mazungumzo
yake na rais Erdogan mradi wa kujenga
sehemu ya kilometa 400 ya reli ya
Standard Gauge (SGR) licha ya kwamba
moja ya makampuni ya Uturuki
yanawania zabuni katika ujenzi wa reli
hiyo itakayounganisha nchi ambazo
hazina bandari.
Kwa upande wake waziri wa Maliasili na
Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na
waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
wamezungumzia mikataba waliyosaini
leo katika sekta za utalii na afya.
Mikataba mingine iliyosainiwa ni kati ya
mashirika ya ndege ya Tanzania na
Uturuki, mashirika ya utangazaji ya nchi
hizo mbili, mkataba wa maendeleo baina
ya Tanzania na Uturuki, Mkataba wa
ushrikiano katika sekta ya elimu na
utafiti, mkataba kati ya shirika la
kuendeleza viwanda vidogo Tanzania
SIDO na shirika la kuendeleza viwanda
vya kati Uturuki, mkataba wa
ushirikiano katika viwanda vya ulinzi na
mkataba wa ushirikiano baina ya chuo
cha diploamsia cha Tanzania na Chuo
cha Diplomasia cha Uturuki.
Rais huyo amefuatana na mkewe mama
Emine Erdogan pamoja na mawaziri
watatu ambao ni waziri wa Mambo ya
Nje, Mevlüt Çavuşoğlu, waziri wa
Uchumi, Nihat Zeybekekci na waziri wa
Nishati na Maliasili, Berat Albayrak
Rais pia amefuatana na wafanyabiashara
wapatao 85 wa nchi hiyo.Taarifa ya
ziara yake imeonyesha kutakuwa pia na
kongamano la kibiashara litakalo waleta
pamoja wafanyabiashara wa pande zote
mbili Tanzania na Uturuki.