Recent Posts

PropellerAds

Sunday, January 29, 2017

Makamando wa Marekani wavamia ngome ya al-Qaeda Yemen

Ripoti kutoka Yemen, zinaeleza kuwa
shambulio, lililofanywa na makamando wa
Marekani, limeuwa watu kama 30,
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Qaeda
na raia.
Hata hivyo jeshi la Marekani linasema kuwa
kamando wake mmoja, aliuwawa, na wengine
watatu walijeruhiwa, katika shambulio dhidi
ya makao makuu ya al-Qaeda nchini Yemen.
Marekani kumsaka mtoto wa Osama
Ndege ya jeshi la Marekani iliyotumika katika
shambulio hilo, ilielezewa kuwa ilitua kwa
kishindo, na kujeruhi wanajeshi zaidi.
Jeshi linasema wapiganaji 14 waliuwawa,
katika shambulio hilo lilofanywa alfajiri,
katika jimbo la al-Baida.
Lakini watu wa huko, wanasema idadi ya
waliouwawa ilikuwa kubwa zaidi, na
wanasema raia kadha pia waliuwawa.
Mwana wa Osama bin Laden asakwa na
Marekani
Wadadisi wanasema, shambulio hilo la
kwanza la aina yake, tangu Rais Donald
Trump kuapishwa, litaonekana kama ishara
ya lengo lake la kutumia nguvu zaidi dhidi ya
makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.