Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter, amesema shambulizi la anga lililowalenga wapiganaji wa kiislamu nchini Libya limeuwa zaidi ya washukiwa nane.
Shambulizi hilo lilitekelezwa na mpiga shaba wa umbali mrefu wa Marekani likielekezwa katika vikundi viwili vya wapiganaji wa kiislamu siku ya Jumatano, katika eneo la jangwa Kusini Magharibi mwa Pwani ya Mji wa Sirte.
Bwana Carter amesema wengi wa waliofariki inaaminika kuwa walikuwa washambuliaji wa mara kwa mara huko Ulaya.
Maafisa wamearifu kuwa shambulizi hilo la anga, lilitekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Libya chini ya Mkataba wa Kitaifa wa Tripoli.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...
5 weeks ago