Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 26, 2017

SERIKALI YAKUSANYA ZAIDI YA BILLION 19 TANGU KUANZA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
George Simbachawene amesema kuwa kwa
kipindi cha kati ya mwezi Mei hadi mwezi
Disemba mwaka jana, serikali ilifanikiwa
kukusanya kiasi cha fedha TZS bilioni 19
katika mradi wa mabasi yaendayo haraka.
Hayo yamesemwa na Waziri
Simbachawene leo jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ikiwa ni siku moja tangu Rais Dkt
Magufuli alipomtaka waziri huyo kwa
kushirikiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
kueleza umma nikiasi gani wamekusanya
ili ifahamike kama mradi huo unaingiza
faida au ni hasara.

Waziri Simbachawene pia ameagiza vikosi
vya ulinzi na usalama kuhakikisha
vinawaondoa wafanyabiashara wadogo
maarufu kama machinga wanaofanya
biashara zao ndani ya eneo la barabara
hiyo kitu ambacho ni kinyume na sheria.
Aidha, wakati huo huo Waziri
Simbachawene amewaagiza Wakuu wa
Mikoa yote nchini kuhakikisha
wanawachukulia hatua za kisheria wazazi
wote wanaotekeleza watoto wao au
kuwatuma kwenda kuwa ombaomba jambo
linalopelekea ongezeko la watoto wa
mitaani.