Wanawake wanaojitoa mhanga nchini Nigeria
wameanza kutumia watoto kuepuka vizuizi
vya ukaguzi, jambo ambalo, serikali nchini
humo inasema linaweza kuwa mwelekeo wa
hatari.
Tahadhari hiyo imekuja baada ya wanawake
wawili waliokuwa wamebeba watoto
mgongoni kufanya mashambulizi ya kujitoa
mhanga katika mji wa Madagali siku 10
zilizopita.
Januari 13 mwaka huu, wanawake wanne
waliokuwa wakijitoa mhanga walifika kwenye
mji wa Maddaggalee katika jimbo la
Adamawa, wawili walitambuliwa na walinzi
waliokuwa katika vizuizi na kutakiwa
kusimama, baada ya mbinu zao kugundulika.
Lakini wengine wawili walifanikiwa kupita
bila ya kugunduliwa. kubeba kwao watoto
kulifanya wasigunduliwe na kuweza
kusababisha maafa yaliyosababisha vifo vya
watu wanne, wao wenyewe kufariki na watoto
wawili pia waliokuwa wamewabeba katika
mawili tofauti.
Kundi la Boko Haram linajulikana kwa
kuwatumia wanawake, hususan wasichana
katika mabomu ya kujitoa mhanga, Hata
hivyo ni mara ya kwanza katika maasi hayo
kutumia watoto wachanga.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
3 hours ago