Vijana wawili wapenzi ambao stori yao
kuhusu ndoa ya bei rahisi waliyofunga
ilizua hisia za watu wengi kwenye
mitandao ya kijamii, sasa wameahidiwa
kulipiwa gharama zote za mapumziko
baanda ya ndoa (honeymoon).
Wilson Mutara (26) na Ann Wambui (24)
kutoka nchini Kenya inaripotiwa kuwa
walifunga ndoa kwa gharama ya Ksh 100
ambayo ni sawa na TZS 2,147 ambapo
gharama hizo zilikuwa kwa ajili ya
kununua pete tu.
Ndoa hiyo iliyotajwa kuwa ya bei rahisi
kuwahi kutokea nchini humo haikua na
sherehe baada ya wawili hao kutoka
kanisani na walivalia fulana walipokwenda
kufunga ndoa.
“Tulikwenda nyumbani tukapika ugali na
sukuma wiki, tukala na tukalala. Hakuna kitu
cha kipekee tulichokifanya katika mapumziko
(honeymoon) yetu” alisema Mutura.
Padri aliyefungisha ndoa hiyo alichapisha
habari hiyo na ndipo mwakilishi wa
Kampuni ya Utalii ya Bonfire Adventure
alipokutana na wanandoa hao.
Kampuni hiyo ndiyo ilijitolea kudhamini
mapumziko ya wawili hao baada ya
kufunga ndoa.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
3 hours ago