Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 26, 2017

PICHA: RAIS OBAMA NA MICHELLE OBAMA WAKIWA MAPUMUMZIKONI KISIWA CHA NECKER.

Michelle Obama katika uwanja wa ndege
wa Palm Springs International Airport,
Jumatatu akienda mapumzikoni visiwa vya
Caribbean.Michelle Obama katika uwanja wa ndege
wa Palm Springs International Airport,
Jumatatu akienda mapumzikoni visiwa vya
Caribbean.Baada ya hapo waliekekea Caribbean
katika kisiwa binafsi kinachomilikiwa na
Bilionea wa Uingereza Sir Richard
Branson, kinachojulikana kwa jina la
Necker. Kama bilionea huyu hayupo
kisiwani hapo, basi nafasi ipo wazi kwa
mtu yeyote kukikodi na kwenda kustarehe
ama kupumzika, kitu ambacho watu wengi
mashuhuri duniani wamekuwa wakivizi
kwa kutokuwepo kwa bilionea huyo ili nao
wakajivinjari. Mastaa kama Mariah Carey,
Robert DeNiro, Princess Diana na
aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela washawahi kwenda mapumzikoni
kwenye kisiwa hicho.
Michelle Obama alipigwa picha akiwa
anapanda kwenye ndege Binafsi ya
bilionea Richard Branson iliyowapeleka
moja kwa moja kisiwani hapo kwa
mapumziko yao.

Baada ya kuwa ikulu kwa miaka nane,
sasa ni ufukweni tu!
Rais Barack aobama na mkewe Michelle
walifika katika kisiwa cha Necker
kinachomilikiwa na bilionea wa Uingereza
Jumatatu kwenye mapumziko
wanayostahili baada ya kumaliza kipindi
cha Urais. Obama na Michelle waliondoka
Wahington D.C siku ya Ijumaa mara baada
ya kuapishwa kwa Donald Trump. Kabla ya
kupanda ndege kwenda mapumzikoni, Rais
huyo wa 44 wa Marekani aliwatania
waandishi, “Michelle na mimi
tumetamani kupumzika kwa muda mrefu
sana, kwahiyo leo sisemi chochote.”
Hawakupoteza muda baada ya kusema
hayo, walipanda ndege yao na kwenda
mapumzikoni.
Kwanza walikwenda Palm Springs,
California, kwa mapumziko mafupi katika
mji wa mapumziko uitwao Rancho Mirage
home unaomilikiwa na James Costos,
aliyekuwa Balozi wa Marekani
nchini Hispania na Andorra wakati wa
utawala wa Obama.