Recent Posts

PropellerAds

Thursday, January 26, 2017

Mwanaume apotea njia na kuendesha baiskeli siku 30

Mwanamume mmoja nchini China ambaye
alikuwa na matumaini ya kuendesha baiskeli
hadi nyumbani kwao kusherehekea mwaka
mpya, aligundua baada ya siku 30 kuwa
alikuwa amepotea njia.
Mwanamume huyo alikuwa na matumaini ya
kuwasil nyumbani kwao huko Qiqihar mkoa
wa Heilongjian baada ya kuanzia safari yake
huk Rizhao umbali wa kilomita 1,700.
Lakini alisimamishwa na polisi wa trafiki
akiwa amepotea umbali wa kilomita 500
katika mkoa wa Anhui.
Wakati waligundua, polisi walimlipia tikiti ya
treni ili arudi nyumbani.
Ripoti zinasema kwa mwanamume huyo
alikuwa akilala maduka ya intaneti kwa
sababu hakuwa na pesa.
Mwanamume huyo hakuwa na uwezo wa
kusoma ramani na hivyo alikuwa akitegemea
watu kumuelekeza.
Polisi walimsimamisha kwa sababu alikuwa
akitumia barabara ambayo baiskeli
haziruhisiwi kuitumia.
Baada ya kugundua makosa yake, polisi na
watu wote waliokuwa kituoni ambapo
alisimama walichanga pesa na kumnunulia
tikiti ili asafiri nyumbani.