Wachimbaji madini 15 wameokolewa wakiwa
hai baada ya mgodi wao kupolomoka siku
tatu zilizopita
Ajili hiyo iliyokea usiku wa kuamkia Alhamisi
iliyopita, tarehe 26 Januari, katika mgodi
uitwao RZ Gold Mine, unaomilikiwa na raia
wa China katika machimbo ya dhahabu
yaliyopo Geita Kaskazini Magharibi mwa
Tanzania
Wachimba mgodi 14 wakwama ndani ya
ardhi Tanzania
Je,kuwa karibu na mgodi ni neema au
la?
Manusura hao ni raia 14 wa Tanzania na
mmoja wa China.
Mwandishi wa BBC Halima Nyanza
aliyeshuhudia zoezi la uokoaji anasema eneo
hilo lilijawa na shangwe na vilio vya furaha
wakati ndugu, jamaa na wachimbaji wengine
walipokuwa wakishuhudia uokoaji wa
manusura hao.
Manusura hao walionokena wadhaifu kiafya,
lakini walipatiwa huduma ya kwanza mara
moja na kisha kupelekwa katika kituo cha
afya kilichopo jirani
Uchunguzi wa nini hasa kilisababisha ajali
hiyo unaendelea, lakini hii si mara ya kwanza
kwa tukio kama hili kutokea
Mwaka jana mwezi Novemba, Tanzania
ilisherehekea ukoaji wa 'kimiujiza' baada ya
wachimbaji watano kuokelewa wakiwa hai
baada ya kukwama chini ya ardhi kwa siku
41.
Eneo la Magharibi mwa Tanzania lina migodi
mingi na wachimbaji wengi hutoka vijiji vya
jirani.
Hata hivyo migodi mingi haikaguliwi mara
kwa mara na hali ya usalama ya migodi hii
haitimizi viwango rasmi.
Naibu waziri wa nishati Dkt Medard
Kalemani, amesema serikali itahakikisha
wachimbaji wana kuwa salama.
Mgodi huo utakuwa chini ya uangalizi kwa
siku tano kabla wachimbaji kuruhusiwa
kufanya kazi.
Naibu waziri pia amewaagiza makamishina
wa madini kufanyia tathmini migodi
mwingine ya wachimbaji wadogo kwa siku
tano, kuanzia kesho
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 22, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 22,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
6 hours ago