Wizara ya ulinzi nchini Uingereza inasema
kuwa ina imani na silaha za nuklia za nchi
hiyo licha ya ripoti ya kutokea hitilafu
wakati wa majaribio.
Gazeti la Sunday Times, linasema kuwa
kombora ambalo halikuwa limebeba silaha
lililirushwa kutoka kwa manowari HMS
Vengeance, karibu na pwani ya Florida
mwezi Juni lilibadili mwelekeo na kuelekea
nchini Marekani.
Majaribio ya awali yaliyofanikiwa yalikuwa
yakitangazwa kwa hata kwa njia ya video,
lakini jaribio hilo halikutangazwa.
Kimya hicho kilizua maswali kuhusu huenda
kulikuwa na hililafu kabla ya kura ya bunge
ya mwezi Julai, ambayo iliiamrisha kutolewa
dola bilioni 50 za kuboresha mpango wa
nyuklia wa Uingereza unaopitwa na wakati.
Albania yatangaza kupiga marufuku TikTok kwa mwaka mmoja
-
Waziri mkuu wa Albania ametangaza kuwa serikali inakusudia kuzuia ufikiaji
wa TikTok kwa mwaka mmoja baada ya mauaji ya mvulana wa shule mwezi
uliopita k...
3 hours ago