Uamuzi wa waziri mkuu wa Uingereza
Bi Theressa May wa kumualika rais Donald Trump wa Marekani umemuweka
malkia katika hali ngumu, kulingana kiongozi wa zamani wa afisi ya
maswala ya kigeni nchini humo.
Katika barua alioandika kwa gazeti la The Times, Lord Rickets amesema kuwa ombi hilo lilifanywa mapema mno.Ombi la kutaka ziara hiyo ya Donald Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali limefaulu kupata zaidi ya saini milini 1.5.
Siku ya Jumatatu, maelefu ya watu nchini Uingereza waliunga maandamano dhidi ya agizo la usafiri la Donald Trump kuhusu mataifa saba ya kiislamu.
Mkakati huo wa uhamiaji wenye utata ulizua mjadala bungeni.
Lord Rickets ambaye alikuwa katibu wa maswala ya kigeni kutoka mwaka 2006-10 alisema kuwa sio jambo la kawaida kwa rais wa Marekani kualikwa kwa ziara ya kitaifa katika mwaka wa kwanza wa utawala wake.
Alihoji iwapo bw Trump alistahili heshima hiyo .
''Ingekuwa vyema kusubiri na kuona ni kiongozi wa aina gani kabla ya kumshauri Malkia kumualika.Sasa Malkia amewekwa katika hali ngumu sana'',aliongezea kiongozi huyo.