Recent Posts

PropellerAds

Sunday, January 22, 2017

Watu 16 wafariki ajali ya basi la shule Italia

Basi lililokuwa limewabeba watoto wa shule
limegonga nguzo ya umemena kushika moto
kaskazini mwa Italia.
Maafisa wa huduma za dharura wanasema
watu 16 wamefariki.
Basi hilo lilikuwa limewabeba wanafunzi
kutoka Hungary na liligonga nguzo ya
umeme lilipokuwa linatoka kwenye barabara
kuu karibu na mji wa Verona Ijumaa usiku.
Maafisa wa huduma za dharura wa Italia
wamesema kwenye Twitter kwamba watu 39
wamejeruhiwa.
Basi hilo lilikuwa safarini kuelekea Budapest
kutoka Ufaransa, ambapo wanafunzi hao
walikuwa wameenda kwa likizo milimani.
Shirika la habari la Italia Ansa limesema
wanafunzi kadha, wengi wavulana,
walirushwa nje basi hilo lilipogonga nguzo
hiyo.
Wengine walikuwa wamekwama ndani ya
basi liliposhika moto, Ansa imeripoti.
Idadi ya waliofariki haitarajiwi kuongezeka,
maafisa wa huduma za dharura wanasema.