Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, January 24, 2017

JE? NI KICHWA GANI UNACHOTUMIA KUFANYA MAAMUZI..?


Na Mwl John C Ntogwisangu_

Mwanaume ana Vichwa viwili, Kimoja kipo juu na kingine kipo chini.

Vichwa Vyote vina Kazi yake na umuhimu wake Katika Mwili, hakuna kilicho bora kuliko kingine.

Vichwa hivi mara nyingi hupingana Katika utendaji wa Kazi.

Wakati kichwa cha juu kinafikiria kwa 100%, kichwa cha chini uwezo wake wa kufikiria huwa 0%.

Ni kwenye tukio moja tu la uumbaji ambapo Vichwa hivi hufanya Kazi kwa kushirikiana, Mbali na tukio hilo mara zote hupingana.

Yusufu alitumia kichwa cha juu, kushinda dhambi ya uzinzi dhidi ya mke wa bosi wake Potifa.

Lakini Daudi kwa kutumia Maamuzi ya kichwa cha chini alijikuta akianguka kwenye uzinzi na mke wa askari wake mwaminifu Uria.

Shujaa wa Israeli alisumbua wafilisti, alimkamata Simba na kumuua kwa kutumia mikono yake tu bila silaha yoyote alijikuta akitobolewa macho na kukamatwa kama kuku pale alipotumia kichwa cha chini kutoa siri yake kwa Delila.

Mtu mwenye Hekima zaidi Duniani aliyewahi kuwepo na na hatakuwepo mwingine mwenye Hekima zaidi yake, Mfalme Sulemani alijikuta AKIOA wanawake 700 na kuwa na vimada rasmi (nyumba ndogo) 300, hata akaacha kumuabudu Mungu na kuabudu miungu migeni, pale alipofikiria kutumia kichwa cha chini.

Historia ya ulimwengu na Biblia inaonesha wanaume wengi jinsi walivyoangamia kwa kusikiliza na kufuata Maamuzi ya kichwa cha chini.

_Hivi unafikiri inakuwaje mwanaume ambaye ameoa tena ana mke wake mzuri tu anafikia hatua ya kulala na mdogo wa kike wa mke wake au kutembea na house girl_❓

_Mzee wa makamo na mwenye heshima zake anapojihusisha kingono na binti ambaye ni sawa na Mtoto wake wa kumzaa_❓

_Hivi inakuwaje pale mwanaume anapoua au kujiua kwa sababu amemkuta mpenzi wake akiwa na mwanaume mwingine_ ❓

_Au mtumishi wa Mungu kuanguka kwenye dhambi na mshirika wake_❓

Yote hayo hutokea pale wanaume tunapoocha kufikiri kwa kutumia kichwa cha juu na badala yake kutumia kichwa cha chini. Loo...! Kweli kichwa cha chin ni Kidanganyifu na kimewaponza wengi.

Maamuzi ya kichwa cha juu huhuzunisha, ni magumu kuyafuata lakini huleta faida ya kudumu na hukufanya umpemdeze Mungu.

Maamuzi ya chini hufurahisha, ni mepesi kuyafuata lakini yenye Madhara ya KUDUMU na hukufanya umkosee Mungu.

_JE, MWANAUME UNAFIKIRI NA KUFANYA MAAMUZI KWA KUTUMIA KICHWA KIPI?_

Bahati ni kwamba, kichwa cha chini mara nyingi huwa kimelala na hakiwezi kufikiria mpaka pale Macho Yaone na kichwa cha juu kifikirie kile kilichoona ndipo kichwa cha chini huamka na kuanza kufanya Kazi.

Ndiyo maana mtumishi wa Mungu Ayubu alisema ameweka agano na macho yake kuwa hatamwangalia mwanamke kwa kumtamani. _Ayubu_ 31:1

Na hii ndio SIRI pekee ya ushindi kwa Wanaume. Kuweka Agano na macho yako kutokumuangalia mwanamke kwa kumtamani.

Mwanaume, kichwa cha chini kisizidi kichwa cha juu Katika Maamuzi na kukuponza kama Samsoni kwa Delila.

*BE SMART.. BE A MAN*

NB : _Lugha iliyotumika ni ya kikubwa na ujumbe ni wa kikubwa, kama haujaelewa ujumbe huu basi oga, ule na ulale.. Waachie wakubwa._

*Nukuu Katika Biblia...!*

Mwanzo 39 :7-12, 2 Samweli sura ya 11, I wafalme 11 :1-3, Waamuzi 16 :4-21