Recent Posts

PropellerAds

Tuesday, February 28, 2017

jinsi ya kutengeneza mfumo wa maisha unaotaka

Image result for win life
Inawezekana una ndoto au mipango ya kuishi maisha ya namna fulani ambayo unayoyataka. Je, kitu cha kujiuliza, ulishawahi kujua utawezaje kushi maisha hayo unayoyataka?

Je, ni mikakati ipi ambayo umeweka hadi uweze kufikia hatua ya kuweza kutengeneza maisha unayoyataka? Kwa kawaida bila hata kuumiza kichwa, yapo mambo ya kuzingatia ili yakusaidie kuishi maisha unayoyataka.

Haya ni mambo ya msingi sana ambayo ukizingatia yatakusaidia uweze kutengeneza maisha bora unayohitaji. Unajiuliza ki-vipi, hapa nikiwa na maana maisha ya ndoto zako, ikiwa lakini utachukua hatua.

Ni mambo gani ambayo unatakiwa kufanya ili kutengeneza maisha ya mafanikio unayoyataka? Hebu fuatana nami katika makala haya ili tuweze kujifunza kwa pamoja.

1. Tambua kitu unachokitaka.
Ikiwa haujui kile unachotaka vizuri kwenye maisha yako, usije ukashangaa ukaendelea kuwa mtu wa kutokuwa na mafanikio karibu kila siku. Kabla hujapata kitu chochote kwenye haya maisha lazima uje ni kipi unataka.

Watu wengi wanakwama sana kwenye maisha kwa sababu ya kutokujua vizuri wanachotaka. Chukua muda wako kidogo ulionao na kisha kitambue kile unachokitaka kwenye maisha yako.

2. Tengeneza mfumo wa kufikia hicho unachokitaka.
Kwa kuwa umeshakijua hicho unachokitaka katika maisha yako, sasa hapa unatakiwa kutengeneza mfumo wa kuhakikisha unakikamilisha kitu hicho. Unatengeezaje huo mfumo? Ni kwa kufanya kila siku.

Acha kusimamishwa na kitu chochote. Weka nguvu za uzingativu na fanya kila siku mpaka malengo yako yatimie. Ikiwa utafanya kila siku, uwe na uhakika baada ya muda utafikia kile unachokitaka.

3. Weka juhudi sana.              
Wakati unapokuwa umejiwekea mikakati ya kudfika kule unakotaka kufika kuna ni rahii tu kujikta unashindwa kufanikisha adhima hiyo ikiwa huataweka juhudu sana.

 Image result for win life

Unatakiwa uweke juhudi kuhakikisha mpaka unafanikiwa. Hakuna kulala katika hilo jitahidi sana ufanye kila linawezekana mpaka kuona kila kitu kinakaa sawa.

4. Weka nguvu za uzingativu kwa hicho unachokifanya.
Usijiruhusu ukawa mtu wa tamaa, wakati upo kwenye harakati za kutengeneza maisha unayoyataka wewe. Kati ya kitu kinachowaangusha watu ni pamoja  na tamaa ya kutaka kufanya mambo mengi kwa pamoja.

Ni muhimu nguvu zako ukaziweka sehemu moja. Hata ikitokea jambo zuri vipi, kipindi ambacho unatengeneza maisha unayoyataka, ukishaweka nguvu ya uzingativu usilifanye jambo hilo. Kitu cha msingi ujifunze kutulia ili kufikia mafanikio yako.

5. Jifunze kila siku juu ya kitu hicho.
Njia ya kufikia mafanikio mara nyingi ni njia ambayo haijanyooka kabisa kama baadhi wanavyofikiri. Zipo changamoto nyingi zinazojitokeza. Kila zinapotokea changamoto hizo amua kujifunza na kujirekebisha kwa kufanya upya kila siku

Pale unapokutana na changamoto za aina yoyote ile hutakiwi kukata tamaa na kutaka kurudi nyuma. Kitu cha muhimu ni kujifunza na kufanya hadi uone umeweza kufikia lengo la kuishi maisha unayotaka.

Unatakiwa uamua kujifunza juu ya kitu ambacho umeamua kukifanya mpaka uwe mtaalamu kabisa tena uliyebobea. Kwa hali, hiyo itakusaidia sana kuweza kuishi maisha unayoyataka.

Mwisho, mtu kuishi maisha anayoyata sio ajali wala bahati. Unaweza ukaishi maisha unayoyataka ikiwa utatengeneza mfumo huo na kuzingatia mambo haya muhimu kama tulivyoyaangalia kwenye makala haya.

Mambo yatakayo kufanya ukose heshima kwenye jamii yako

Image result for disrespect picture 
Hakuna kitu kibaya maishani kama kuonekana upo katika daraja la chini na mtu wa kudharaulika kwenye jamii unayoishi. Kisaikolojia kuna madhara makubwa.

Ni imani yangu kuwa kila mwanadamu timamu anapenda kuheshimiwa lakini wengi wetu tunashindwa kupata heshima tunayoitaka kwa sababu hatufahamu jinsi ya kuishi mbele ya wenzetu.

Kitaalamu, hakuna jambo ambalo hutokea maishani bila sababu maalumu hivyo hata kudharauliwa kwako au kwetu ndani ya jamii tunayoishi kunatokana na jinsi tunavyoenenda.

Njia za kukusaidia kurejesha heshima yako kwa kuperuzi na wewe baadhi ya dokezo muhimu zinazoweza kukusaidia kujitambua na kuweza kuyaepuka maisha ya kudharauliwa.

1. Muonekano.
Kwanza kabisa ni jinsi unavyoonekana. Muonekano ninaouzungumzia hapa ni usafi wa mavazi na mwili kwa ujumla. Hata siku moja hakuna mchafu anayeheshimika katika jamii anayoishi hata kama ana kipaji kikubwa kiasi gani.

Kwa hiyo uchafu wa mavazi na mwili huchangia mtu kudharauliwa katika jamii anayoishi.

Linaweza kuwa jambo dogo sana lakini ni moja kati ya sababu kubwa inayochangia kuporomoka kwa thamani yako mbele ya wenzako.

2. Mazungumzo.
Hapa naomba nieleweke kuwa unachokizungumza kinaweza kukujengea heshima au kukubomolea heshima. Kauli zisizo na busara zitakufanya udharaulike kwa kila mtu. Uropokaji usiokuwa na mantiki huchangia kuporomosha heshima yako hasa kama utakuwa muongeaji zaidi. Biblia inasema penye wingi wa maneno hapakosi uovu.

3. Utendaji wako wa Kazi.
Ndugu zangu, siku zote heshima ya mtu ni kazi. Watu wengi hawapendi kufanya kazi kwa bidii huku wengine wakijiendekeza kwa tabia ya kuombaomba, jambo hilo halifai kwa vile huchangia kubomoa heshima yako mbele ya jamii. Fanya kazi usiishi bila kujishughulisha.

4. Kutotimiza ahadi.
Kama una tabia za kuahidi mambo halafu unashindwa kuyatekeleza, basi unajiweka katika nafasi mbaya ya kutunza heshima yako katika jamii unayoishi. Bora ukwepe kutoa ahadi kuliko kuahidi na kutotimiza.

5. Sifa zisizo na maana.
Nakumbuka msemo mmoja kutoka kwa mwandishi mwandamizi aliyekuwa mtaalamu wa falsafa za maisha, marehemu Adolf Balingilaki, ambao unasema kwamba: “Ukitafuta heshima kwa gharama ya juu, basi utalipwa dharau kwa bei nafuu.”

Msemo huu unamaanisha nini? Siku zote ukiwa unafanya mambo yako kwa ajili ya kusifiwa au mazungumzo yako kuwa ya kujiinua, watu watakudharau.

6. Kutokuwa mwaminifu.
Suala la uaminifu ni pana, kuna uaminifu wa fedha, siri, dhamana na mambo kama hayo, hivyo ni vema kila unachoaminiwa lazima ukitunze kwani ukiwa mtu wa kuvunja uaminifu fahamu kuwa utashusha heshima yako

Chanzo Cha Hofu Nyingi Ulizonazo Na Zinazokuzuia Ushindwe Kufanikiwa

Image result for people with fear picture
Wapo watu ambao ni waoga sana kuwajibika hasa linapokuja suala la kufanya kile kitu wanachotakiwa kufanya. Utakuta ni watu wa kusingizia sana hiki au kile, kwamba siwezi kufanya kwa sasa, kwa sababu hii au ile.

Kwa mfano, utakuta mtu anataka kuanzisha biashara ya aina fulani, ambapo ukiangalia kama ataanzisha biashara hiyo, itamsaidia sana mtu huyo kuweza kuingiza kipato kikubwa na cha ziada.
Hata hivyo, kitu cha kushangaza au cha ajabu kwa sababu ya hofu ama wasiwasi tu, mtu huyo atajikuta anatoa visingizio vingi sana mpaka kushindwa kuanza biashara hiyo, ambayo ilitakiwa ainze mara moja.

Kitu usichokijua, kisaikolojia unaposhindwa kufanya jambo fulani kwa sababu ya hofu za mara kwa mara, mawazo yako ya ndani, mawazo yanayoumba au kupelekea mambo hutokea, huchukua hofu hiyo na kuihifadhi na kuifanya kama ‘ulemavu’ wako.

Kwa hiyo kila unapojaribu kufanya jambo jipya utakuta wazo linashuka haraka sana ndani yako, ‘Je ukishindwa itakuwaje? Si unaona wengi sana huwa wanashindwa hapo,’? Utashangaa ubongo wako una hofu sana, hata pengine bila kujua kwa nini?.

Lakini ukiangalia, hiyo yote inatokana na hofu ndogo ndogo ambazo ulizibeba sasa zimekaa kwenye mawazo yako ya kina na imekuwa kama ndio ‘ulemavu’ wako wa kiakili yaani 'psychological disorders', sasa kila kitu ukitaka kukifanya unakuwa una hofu.

Kitu cha kujiuliza kwa nini watu wanakuwa na hofu sana hasa pale wanapotaka kuanza jambo fulani? Chanzo hasa huwa nini?

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea hofu moja kwa moja kwenye maisha yako na kushindwa kuchukua hatua sahihi za majukumu yako.

1. Kuogopa kukosea.
Utakuta hapa hofu inazalishwa sana kwa sababu ya kuogopa kukosea. Utakuta mtu anakuwa ana wasi wasi mwingi hivi jambo hili lisipokwenda sawa itakuwaje? Mwisho wa siku kila kitu hufika mahali kimekwama.

2. Kuogopa kushindwa.
Pia kuna watu ambao wanajawa na hofu kwa sababu ya kuogopa kushindwa. Kwa watu kama hawa kwao wanaona inakuwa ni bora wasifanye kabisa kuliko wakafanya halafu wakashindwa. Kwa lugha rahisi watu wenye hofu hii huwa hawafanikiwi.

3. Kutokujiamini.
Unaposhindwa kujiamini, elewa kabisa huwezi kufanikiwa katika kitu chochote. Kujiamani mara nyingi ndio msingi wa mafanikio. Waangalie watu ambao wanajiamini utakuta ni  watu ambao wanamafanikio wakati wasiojiamini hawana kitu maishani mwao.

4. Kuogopa ushindani.
Mwingine utakuta anashindwa kuanza jambo analotakiwa afanye, inaweza kuwa biashara au kitu chochote eti kisa kwa sababu ya kuogopa ushindani. Kwa jinsi anavyoogopa ushindani anajikuta hawezi tena kufanya kitu.

5. Kukosa hamasa.
Pia ni rahisi sana kuanza kuingiwa na hofu kama umekosa hamasa ya kile unachokifanya. Ni muhimu sana kuwa na hamasa ili ikusaidie kukujaza ujasiri wa kufanya hicho unachokifaya kwenye maisha yako.

6. Mawazo hasi.
Kama una mawazo sana kama vile ‘aah mimi sina uwezo wa kufanikisha hili, huu mradi sio saizi yangu,’ uwe na uhakika hutaweza kufanya kwa ujasiri, hapo utakuwa unajijaza hofu mwenyewe zitakazo kufanya ushindwe tu.

Kimsingi, kuogopa kushindwa, kuogopa ushindani, kugopa kukosea, kukosa hamasa, mawazo hasi na kutokujiamini ni moja ya sababu zinazokufanya wewe uwe na hofu kubwa kwenye maisha yako.

Mitandao ya kijamii inaweza kusababisha magonjwa ya akili - Utafiti

Image result for mobile features
Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook, Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na mingineyo kila siku?

Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi.

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi.

Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.

tiba ya jino linalouma hii hapa

Image result for teethMeno ni muunganiko wa mfupa wa jino, Fizi na Mishipa. Maranyingi watu wengi huwa pale wanapoumwa na jino wanakimbilia kung’oa jino eti dawa ya jino kuling’oa jambo ambalo si kweli.

Tambua ndugu yangu kuwa unapokwenda kung’oa jino unang’oa Mfupa sio Fizi wala mishipa ambayo hakuna madhara kwa bakteria anaesababisha jino kuuma.

Tambua kuwa kwenye kinywa cha mwanadamu kuna bakteria wanaoishi mdomoni wanaitwa NORMAL FRALER. Bakteria hawa ndio wanaotengeneza ute wenye Acid unaolainisha chakula kwa haraka mdomoni. Na ndio kazi yao.

Lakini wanasababisha ugonjwa unaoitwa GINGIVAITES, ugonjwa huu husababisha fizi kutoa damu haswa unapopiga mswaki, lakini ukiachwa ukawa sugu unasababisha ugonjwa wake kuwa sugu na hujulikana kama MACHODIFECE ugonjwa huu husababisha na hufanya meno kuoza, ama kutoboka kutokana na bakteria AFINOTOBALASAD ndio wanaosababisha na huwa wanaingia ndani kwenye fizi kwa ajili ya kula damu. Hapo ndipo mtu hupatwa na tatizo la  kuumwa na jino au meno.

 Ili kuondoa tatizo hili, ni lazima uwaue hao bakteria na si kong’oa jino kwani wadudu hao walivyo unapong’oa jino moja wao huwa wanahamia jino jingine.

Tiba rahisi ya jino au meno yanayouma bila kung'oa wala kutumia dawa za hospitali tumia mojawapo kati ya hizi hapa:

Tengeneza na kunywa juisi ya bilinganya (Bringal).
Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.

Image result for teeth
Saga majani makavu ya mint kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.

Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka wool hiyo kwenye jino linalouma.

Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma

DAWA ZA NYWELE ZINAZOSABABISHA UVIMBE WA KIZAZI KWA WANAWAKE

Image result for women washing hair
Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

“Kemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,” anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

“Zipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,” anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

“Dawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,” anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.
 
Image result for women washing hair
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa “Lye Relaxer” ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa “No Lye Relaxer” yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa ‘no lye relaxer’ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa “Lye Relaxer”.

Trump amlaumu Obama kwa maandamano

Trump amlaumu Obama kwa maandamano
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kuwa Barack Obama ndiye anahusika na maandamano dhidi ya uongozi wa Republican.
"Nafikiri Rais Obama anahusika kwa sababu ni watu wake wanaohusika kwenye maandamanohayo," Trump alikiambia kituo cha Fox News.
Trump alikuwa akiongea na kituo cha Fox News
Trump hakutoa ushahidi wowote kwa madai yake na Obama bado hajajibu lolote.
Trump pia alizungumzia bajeti na masuala mengine.Alipoulizwa kuhusu maandamano yanayohusu amri ya kusaka. alisema kuwa ni wafuasi wa Obama waliohusika.
 Trump anasema ataongeza bajeti ya jeshi kwa asilimia 10

Uganda yaongoza kwa ufasaha wa lugha ya kiingereza Afrika

Uganda imetajwa kuwa nchi yenye raia wanaozungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha zaidi barani Afrika
Utafiti uliofanywa na shirika la lugha duniani World Linguistic Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika Kusini ikiwa katika nafasi ya tatu na Kenya katika nafasi nne.




Kulingana na gazeti la The New Vison nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya video iliomuonyesha malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea kiingereza.
The New Vison linasema kuwa mwaka 2015, mmoja wa malkia hao wa Urembo katika shindano la Malkia wa urembo nchini Rwanda Uwase Honorine alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na majaji wa shindano hilo.
Rwanda iliokuwa chini ya koloni ya Ufaransa ilianza kuzungumza Kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa.
Gazeti la The New Vision linasema kuwa kiingereza nchini Uganda ndio lugha rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini humo.
Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi.
The New Vison linasema kuwa hivi majuzi serikali iliziagiza shule kufunza lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini ikasisitizia kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala.
Mataifa yanayozungumza kiingereza kwa ufasaha:
1.Uganda
2. Zambia
3. South Africa
4 . Kenya
5. Zimbabwe
6. Malawi
7. Ghana
8. Botswana
9. Sudan

unyanyasaji wa watoto wahamiaji libya wakithiri

UNICEF inasema kuwa watoto hunyanyaswa Libya katika harakati za kuelekea Itali
Umoja wa Mataifa umeonya kwamba idadi kubwa ya watoto wanaendelea kuhatarisha maisha yao, kwa kuvuka bahari ya mediterania kutoka Libya hadi Italia.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, linasema watoto 26,000, wengi wao wakiwa bila walezi, walivuka bahari ya mediterania mwaka jana.
Idadi hiyo ni mara dufu ikilinganishwa na mwaka 2015.
 Watoto hukabiliwa na tisho la kufnywa makahaba na magenge ya uhalifu
Katika ripoti mpya, UNICEF, inasema watoto hao wanadhulumiwa na kunyanyaswa kimapenzi na walanguzi wa binadamu, japo huwa hawatoi ripoti kwa polisi kwa hofu ya kutiwa mbaroni na kurejeshwa Libya.

Space X kuwasafirisha watalii 2 mwezini 2018

Watalii wawili kwenda mwezini 2018
Kampuni ya kibinafsi ya kurusha roketi imetangaza kwamba watalii wawili wamelipa kupelekwa mwezini.
Safari hiyo itafanyika 2018 kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya SpaceX Elon Musk, alieongezea kwamba watalii hao tayari wamelipa kiasi fulani cha fedha.
''Hatua hiyo inatoa fursa kwa binaadamu kurudi katika anga za juu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45'',alisemaWawili hao ambao majina yao hayakutajwa wataelekea mwezini wakiwa katika meli hiyo ya angani ambayo itafanyiwa jaribio lake la kwanza la kurusha rekoti isiokuwa na rubani.
Bwana Musk alisema kuwa ushirikiano wa shirika la sayansi na teknolojia ya angani nchini Marekani Nasa umefanya ufanisi wa safari hiyo
 Roketi itakayotumika kuwasafirisha watalii hao
Amesema kuwa abiria hao wawili watasafirishwa kwa kasi zaidi ya watu wengine wowote kuwahi kusafirishwa katika sayari.
Bwana Musk hatahivyo amekataa kuwataja abiria hao wawili ,akisema kwamba ni watu wanaojuana na kwamba hawatoki Hollywood.
Kama wanaanga wa Apollo, wawili hao watasaifiri angani wakibeba matumaini na ndoto za binaadamu wote wanaopenda kusafiri.
Tunataraji kuwafanyia ukaguzi wa kiafya kabla ya kuanza kuwafunza baadaye mwaka huu.

Mkuu wa majeshi afutwa kazi Gambia

Gambia
Rais wa Gambia Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie.
Jenerali Badjie alitangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.

Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana.
Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.

Sunday, February 26, 2017

Tumbili 57 wauawa kwa sababu ya ubaguzi Japan

Tumbili wa barafu wa Japan
Hifadhi moja wa wanyama ambayo ni ya kuwahifadhi tumbili wa barafu imewaua tumbili 57, ambao ilikuwa ikiwahifadhi baada ya kugundua kuwa nyani hao walikuwa na maumbile ya kijenetiki ya familia tofauti .
Hifadhi hiyo ya Takagoyama ilichukua hatua hizo baada ya uchunguziwa DAN kuonyesha kuwa theluthi moja ya tumbili walikuwa na jenetiki ya familia nyingine ambayo haitambuliwi kuwa ya asilia nchini Japan.

Afisa mmoja alisema kuwa tumbili hao walikuwa ili kulinda familia za asili.
Nyani hao waliuawa kwa kudungwa sindano yenye sumu na msimamizi wa hifadhi akawaandaa maombi kwenye hekalu lililokuwa karibu.

Tanzania kuimarisha biashara na Uganda

Rais Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli
Serikali ya Tanzania imesema kuwa itaimarisha biashara yake na Uganda kwa lengo la kuinua uchumi wa raia wa mataifa hayo mawili.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa tayari Tanzania imeanza kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambayo itakwenda pamoja na ujenzi wa bandari kavu Mkoani Mwanza ili kuwapunguzia muda wa usafiri wafanyabiashara wa Uganda wanaolazimika kusafiri hadi bandari ya Dar es Salaam kuchukua mizigo yao inayotoka nje ya nchi kwa meli.
Aidha amesema kuwa serikali yake itakarabati meli ya MV Umoja itakayovusha mizigo hadi bandari ya Port Bell kupitia ziwa Viktoria, mbali na kununua ndege 6 za kusafirisha kwa ajili ya Shirika la ndege la Taifa (ATCL) na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kufikia 3.
"Uwekezaji wa wafanyabiashara wa Uganda hapa nchini Tanzania una thamani ya dola za Marekani milioni 46.05 na umezalisha ajira 1,447"
"Watanzania wanaoishi Uganda ni wengi kuliko wanaoishi katika nchi nyingine yoyote duniani, hii ina maana tunapaswa kushirikiana zaidi na kufanya biashara zaidi"
Kuhusu mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema Tanzania ipo tayari kuanzisha ujenzi huo baada ya kukamilisha mazungumzo ya masuala machache yaliyokuwa yaliosalia na ametaka wawekezaji waanze kazi badala kutoa visingizio.
Kwa upande wake Rais Museveni amemshukuru Rais Magufuli kwa mapokezi mazuri aliyoyapata akisema Uganda itaendelea kuwa ndugu na rafiki wa kweli wa Tanzania huku akisisitiza kuwa rafiki na ndugu wa kweli ni lazima wawe wamoja katika maamuzi na mipango mbalimbali ikiwemo maendeleo na biashara.
Vilevile Rais Museveni ametoa wito kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima kuzungumza lugha moja na kuwa na msimamo wa pamoja ili kukabiliana na ukoloni ambao huko nyuma ulitawala kutokana na watawala wa Afrika kukosa umoja.
Kuhusu bomba la Mafuta, Rais Museveni amesema atafuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo hasa baada ya uamuzi kufanyika kuwa bomba la mafuta yaliyogundulika Hoima nchini Uganda litapitia Tanzania hadi bandari ya Tanga.

Wednesday, February 22, 2017

Mbona bado kuna njaa duniani?

Wanawake wakisubiri huduma ya afya jimbo la Unity Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umetangaza njaa sehemu kadha nchini Sudan Kusini, ambayo ni ya kwanza kutangazwa popote pale duniani katika kipindi cha miaka sita.
Pia kuna onyo la kutokea njaa kaskazini mashariki mwa Nigeia, Somalia na Yemen. Lakini ni kwa nini bado kuna njaa, na ni kitu gani kinastahili kufanywa.
Ni kipi kinaendelea nchini Sudan Kusini?
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa watu 10,000 wanakumbwa na njaa nchini Sudan Kusini na wengine milioni moja wanatajwa kuwa walio kwenye hatari ya kukumbwa na njaa.
Kwa ujumla Umoja wa mataiafa unasema kuwa watu milioni 4.9 au asiimia 40 ya watu wote nchini Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura.
Chanzo kikuu cha njaa ni mzozo. Nchi hiyo imekumbwa na vita tangu mwaka 2013 ambapo zaidi ya watu milioni 3 wamelazimika kukimbia makwao.
Uzalishaji wa mazao umeathiriwa pakubwa na mzozo hata katika maeneo ambayo yamekuwa yakizalisha mazao mengi baada ya mzozo wa viongozi wa kisababisha kung'angania madaraka pamoja na mali asili miongoni mwa makabila.
Ugavi wa chakula Somalia

Tangazo hilo la njaa ni kumaanisha nini?

Njaa inaweza kutangazwa tu wakati idadi ya vifo na viwango vya utapiamlo vinafikia kiwango fulani, kwa mfano:
  • Ikiwa takriban asilimia 20 ya familia zinakumbwa na uhaba mkubwa wa chakula.
  • Viwango vya utapiamlo vinazidi asilimia 30.
  • Na vifo vinazidi zaidi ya watu 2 kwa siku kati ya watu 10,000.
  • Sehemu zinazokuwa na uhaba wa chakula
    Njaa za awali ni pamoja na kusini mwa Somalia mwaka 2011, ya kuisni mwa Sudan mwaka 2008, ya Gode eneo a Kisomalia nchini Ethiopia ya mwaka 2000, Kore Kaskazini mwaka 1996, Somalia kati ya mwaka 1991 na 1992 na Ethiopia kati ya mwaka 1984 na 1985.

    Ni kipi kinaweza kufanywa Sudan Kusini?

    Ni vitu viwili vinaweza kufanywa ili kukabiliana hali hiyo: misaada zaidi ya kibinadau na kutoa fursa ya kufikiwa kwa maeneo yaliyoathirika zaidi
     Watu wengi nchini Sudan Kusini wanaishi kwenye kambi
    Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema kuwa serikali ya Rais Salva Kiir imekuwa ikizuia chakua cha msaada kuenda maeneo mengine. Imeripotiwa kuwa misafara ya misaada na maghala yamekuwa yakishambuliwa.
    Licha ya serikali kukana madai hayo, Rais Kiir kwa sasa ameahidi kuwa misaada yote ya kibinadamu itawafikia watu wanaohitaji kote nchini .

    Mbona kuna uhaba wa chakula maeneo mengini?

    Chanzo kikuu ni mizozo.
    Yemen, kaskazini mashariki mwa Nigeria na Somalia ni sehemu ambapo mapigano yamevuruga vibaya amani na maisha ya kawaida.
    Nchini Yemen mzozo umevutia mataifa jirani na kusababisha uharibifu mkubwa na kuzorota kwa uchumi.
    Nigeria na Somalia zimekumbwa na makundi ya kigaidi hali ambayo imesababisha kuhama kwa watu wengi, kuvuruwa kwa sekta ya kilimo na shughuli zingine kama biashara.
    Watu nchini Yemen wamekumbwa na ukosefu wa maji Ugaidi kaskaziniamashariki mwa Nigeia umesababisha njaa
     

Wabunge waidhinisha kilimo cha bangi Uholanzi

Amsterdam, Netherland
Bunge la chini nchini Uholanzi limeidhinisha kuhalalishwa kwa kilimo cha bangi.
Mswada huo ulioidhinishwa, utawakinga wakulima wa bangi ambao wanatimiza masharti fulani dhidi ya kuadhibiwa.
Mswada huo bado haujaidhinishwa kuwa sheria, kwani utahitaji pia kuungwa mkono na Bunge la Seneti.
Ununuzi wa viwango vidogo vya bangi katika 'migahawa' unakubalika nchini Uholanzi.
Hata hivyo upanzi wa mmea huo na kuuzia kwa wingi migahawa ni kinyume cha sheria.
Migahawa hiyo hulazimika sana kununua bangi kutoka kwa walanguzi.
Mswada huo wa Jumanne ulifikishwa bungeni na mbunge wa chama chenye msimamo wa kutetea uhuru wa raia cha D66, ambacho kwa muda mrefu kimetetea kuelegezwa kwa masharti kuhusu kilimo cha bangi.
Mswada huo uliungwa mkono na wabunge 77 dhidi ya 72, licha ya mwendesha mashtaka wa umma kueleza wasiwasi kwamba kuhalalisha kilimo cha bangi kutaifanya Uholanzi kukiuka sheria za kimataifa.
Wizara ya Afya pia ilikosoa mswada huo.
Hata hivyo, wengi wanasema huenda ikawa vigumu kwa mswada huo kupitishwa katika Seneti, iwapo maseneta watapiga kura kwa msingi wa vyama.
Lakini licha ya shaka kuhusu hatima ya mswada huo, wadau katika sekta ya bangi wamesema wamefurahishwa na ufanisi huo.
"Ni habari njema kwa sekta ya migahawa kani hatimaye - iwapo itapitishwa na Bunge la Seneti - itafikisha kikomo mambo mengi ambayo hatuwezi kuyafanya kwa mpangilio na kwa uwazi," Joachim Helms, mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Migahawa, aliambia shirika la habari la Associated Press.