Aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa
mataifa bwana Kofi Annan amemkosoa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kwa
kuwania muhula wa tatu.
Bw Annan amesema Nkurunziza anafahamu
vyema kuwa ni kinyume cha katiba ya taifa hilo kuwania madaraka kwa
zaidi ya vipindi viwili.Raia huyo wa Ghana anamlaumu rais Nkurunziza kwa kusababisha maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu mia nne.
Bw Annan ameiambia BBC kuwa bw Nkurunziza haoneshi dalili zozote za kutafuta suluhu la amani wala nia ya kutaka mazungumzo ya kweli na wapinzani wake.
Katibu huyo wa zamani ameiomba jamii ya imataifa kuyasaidia mataifa ya Afrika yanayokabiliwa na matatizo chungu nzima kama vile Ethiopia inayokabiliwa na baa la njaa
Annan anasema kuwa mataifa hayo ya Afrika yamesahaulika huku kurunzi ya ulimwengu ikiangazia Syria na mataifa ya Mashariki ya kati.