Mji wa Augsburg Ujerumani umeweka taa za barabarani chini kwenye barabara ili watumizi wa simu aina ya smartphone hawatolazimika kunyanyua nyuso zao kuangalia iwapo taa zimewaka kuvuka barabara.
Taa hizo zilizo nyekundu kama ilivyo kawaida ya taa za barabarani zinapoashiria mtu au magari kusimama, zinaamanisha kwamba watu zaidi watatembea wakiwa nyuso zao zinaangalia chini, lakini bado wataweza kuona wakati sio salama kutembea.
Kifo cha mtoo mwenye umri wa miaka 15 kililazimisha kuwekwa taa hizo, vyombo vya habari vinaarifu.
Aligongwa kwa treni alipokuwa amezubaa na simu wakati akivuka, polisi inasema
Watu wanaotembea huku wakizubaa na simu zao wamepewa jina smombies - jina linalotokana na maneno smartphone na zombie.
Jina hilo ni maarufu sana Ujerumani ambako limetajwa kuwa neno la vijana lililotumika zaidi 2015.