Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
amezichoma pembe za ndovu katika juhudi za kuonyesha taifa lake kuhusu
umuhimu wa kuwahifadhi ndovu.
Zaidi ya tani 100 za pembe za ndovu
zilikusanywa katika mbuga ya wanyama ya Nairobi ambapo zinatarajiwa
kuchomeka kwa siku kadhaa.Pembe hizo zinawakilisha karibia pembe zote zilizopatikana na serikali zikidaiwa kutoka kwa takriban ndovu 6,700.
Hatahivyo wengine wametofautiana na hatua hiyo ya Kenya wakisema inaweza kuongeza visa zaidi vya uwindaji haramu.
Kabla ya kuwasha moto huo,Bw Kenyatta alisema: Wingi wa Pembe hizi ndio unaotupatia shinikizo zaidi kukabiliana na visa vya uwindaji haramu.
''Hakuna na narudia hakuna mtu aliye na sababu ya kushiriki katika biashara ya pembe za ndovu''.