Kenya imeilaumu Tanzania kwa
kuwaweka raia wa Ethiopia katika eneo lake la mpaka siku ya Jumanne
badala ya kuwarudisha makwao kulingana na ripoti ya gazeti la The
standard nchini Kenya.
Raia hao wa Ethiopia walikuwa wamewachiliwa huru baada ya kuhudumia vifungo vya mashtaka tofauti ya uhalifu nchini Tanzania.Maafisa wa polisi wameagizwa kutowaruhusu wageni hao kuingia nchini Kenya.
''Watarudishwa nchini Tanzania walikotoka.Kisa hicho hakikubaliki na hakiruhusiwi na sheria'',Afisa wa Kenya Henry Wafula alinukuliwa akisema