Mwanafunzi ambaye awali alikataa
kulishtumu kundi la wapiganaji wa Islamic State amechaguliwa kuwa rais
wa muungano wa kitaifa wa wanafunzi nchini Uingereza.
Mali Bouattia,ambaye ataanza kuhudumu kuanzia mwezi Septemba pia amekitaja chuo kikuu cha Birmingham kuwa cha Kizayuni.Katika kanda ya video ya 2014 anaonekana akiwataka waislamu kuwasaidia Wapalestina kupinga unyanyasaji wa aina yoyote.
Bi Bouttia atakuwa rais wa kwanza wa muungano huo aliye muislamu na mtu mweusi.
Waziri wa chama cha Leba na aliyekuwa kiongozi wa Wes Streeting alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter akisema Muungano huo hauwawakilishi wanafunzi ipaswavyo.
Mnamo mwezi Octoba wakati bi Boutia alipoajiriwa na muungano huo kama afisa wa wanafunzi weusi, alikataa mjadala uliowasilishwa na wanafunzi wengine kushtumu vitendo vya ugaidi vinavyotekelezwa na kundi la wapiganaji wa IS.
Pia amenukuliwa akisema kuwa mazungumzo ya amani katika eneo la mashariki ya kati yanasaidia miradi ya wakoloni pekee.
Kampeni yake imeshirikisha: Kwa nini mtaala wake ni mweupe? Huku akipinga mipango ya serikali ya kukabiliana na ugaidi.