Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alikutana na Askofu mkuu wa Canterbury na kuibua maswali kuhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Askofu
mkuu Justin Welby amesema alimjibu kiongozi huyo kwamba kuna mitazamo
tofauti kuhusu ndoa hizo miongoni mwa waumini wa kanisa la Kianglikana
kote duniani.Aliongeza hata hivyo kwamba wengi wa waumini wanaamini ndoa ni uhusiano wa muda mrefu baina ya mwanamume na mwanamke.
Askofu Welby alisema ni makosa kuwahukumu au kuwaadhibu watu kwa sababu ya msimamo wao kijinsia na kimapenzi.
Hata hivyo, amesema dalili zilionesha Bw Mugabe hakukubaliana naye.
“Sidhani itakuwa haki kusema kwamba Bw Mugabe alikubaliana name kabisa,” alisema Askofu Welby.
- Mkuu wa kanisa Anglikana agundua babaake sio Welby
- Mugabe: Ninaweza kukutwanga ngumi
- Mbunge ashtakiwa kumtusi mke wa Mugabe
Msemaji wa Lambeth Palace amesema mpango huo ulipangwa dakika za mwishomwisho na ulidumu chini ya saa moja.
Bw Mugabe ni Mkatoliki na hupinga sana ndoa za wapenzi wa jinsia moja.