Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Haki za Kibinadamu ameshutumu sera za mgombea urais
wa chama cha Republican nchini Marekani, akisema ni
sawa na ushenzi.
Zeid Raad al-Hussein, ingawa hakumtaja Bw Trump
moja kwa moja, alizungumzia hatua ya mfanyabiashara
huyo tajiri kutoka New York kuunga mkono mateso
pamoja na sera zake kali dhidi ya Waislamu.
“Ushenzi na ulokole si thibitisho la uongozi thabiti,”
Hussein alisema.
Kamishna huyo pia amekosoa mpango wa mgombea
mwengine Ted Cruz wa kuweka mpango wa kupeleleza
maeneo wanamoishi Waislamu.
“Kutoa matamshi ya chuki, kuchochea na kuwatenga
wengine si jambo la kuburudisha watu nalo, au jambo
la kujifaidi kisiasa,” Bw Hussein ameambia hadhira
katika mji wa Cleveland, Ohio.
Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Ameongeza: "Mmoja wa wagombea wanaoongoza katika
kinyang’anyiro cha kutaka kuwa rais wa nchi hii
alitangaza, miezi kadha iliyopita, kujitolea kwake
kutumia mateso (…) kuumiza watu wengine, ili watoe
habari au wabuni habari ambazo hawazo nazo.”
Wakati wa kampeni, bw Trump alisema kwamba mateso
wakati mwingine hufanikiwa na akaahidi kurejesha njia
hatari zaidi kuliko kutumia maji kulazimisha washukiwa
kufichua habari.
Njia hizo zilitumiwa na jeshi la Marekani katika
washukiwa wa ugaidi lakini zilipigwa marufuku na
utawala wa Bw Obama.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 9, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 9,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
27 minutes ago