Recent Posts

PropellerAds

Thursday, April 28, 2016

Anonymous wavamia mtandao wa wizara Kenya

 Anonymous
Kundi la wadukuzi wa mitandaoni la Anonymous limeshambulia tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Kenya na kuiba data muhimu, tovuti moja ya usalama mtandaoni imeripoti.
Shambulio hilo lilitekelezwa chini ya operesheni iliyopewa jina OpAfrica, ambayo lengo lake ni kukabiliana na udhalilishaji wa watoto, kufanyishwa kazi kwa watoto na ufisadi katika nchi za Afrika, tovuti ya HackRead imeripoti.
Operesheni hiyo ilizinduliwa mwaka jana.
Serikali ya Kenya haijasema iwapo kuna nyaraka na habari muhimu ambazo zimeibiwa na wadukuzi hao.
Tovuti ya HackRead inasema data ya jumla ya 1TB ambayo imeibiwa imeanikwa kwenye “mitandao ya giza” ambayo ni mitandao ambayo ina siri kuu na huficha majina na utambulisho wa wanaoitumia.
Anonymous majuzi walidukua tovuti ya kampuni ya kusafisha mafuta ya Kenya pamoja na tovuti za mashirika mengine yanayomilikiwa na serikali.
Udukuzi wa tovuti nyingi katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara hata hivyo sana huhusisha kuzichafua badala ya kuiba data.
Huku watu na serikali nyingi zikianza kufanya shughuli zaidi mtandaoni, kuna habari na maelezo mengi zaidi ambayo yanaweza kuandamwa na wadukuzi.
Anonymous hufanya kazi kama mtandao wa ushirika. Hushirikisha wadukuzi kutoka nchi mbalimbali ambao hutumia jina hilo na hivyo huwa vigumu kufahamu iwapo wadukuzi wanatoka nje ya nchi au ndani ya nchi.
Kundi hilo hujidai kuwa la wanaharakati ambao hutekeleza uvamizi wa mitandaoni kukabiliana na ufisadi na ukiukaji wa haki.

Related Posts:

  • God Will Sustain You a Day at a Time Earlier this year, my arms completely gave out as I was getting ready. I couldn’t even get dressed by myself. I was exhausted, and it wasn’t even nine in the morning. I suffer from post-polio syndrome, and I’m never sure wh… Read More
  • Live Like Death Is the Beginning Where did Abraham find the faith to lay his one and only son on the altar? He did not lay his incarnate promise on the altar because it made sense or he could prove it doctrinally or because the promise was dispensable. A… Read More
  • Does Junk Food Dishonor God? Giving Thanks for Junk Food? Good question. Here’s my answer in a couple of sentences, and then I’m going to just kind of ramble. I want to talk Bible here, but that is kind of hard. You’ll see if it helps. Here’s my answ… Read More
  • The Cost of Redemption The shortest verse in the Bible is John 11:35: “Jesus wept.” But for all its grammatical simplicity, it’s packed with unfathomable complexity. Jesus wept after speaking with Lazarus’s grieving sisters, Martha and Mar… Read More
  • How Do I Overcome Sin? How do you stop committing a certain sin? Some suggestions may involve putting guardrails up around areas of temptation or being held accountable by trustworthy friends. Others include conditioning your mind to be better or… Read More