Recent Posts

PropellerAds

Thursday, April 7, 2016

FELEX NTEBENDA:MARUFUKU VIROBA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga
marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa
huo.
Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni
nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa
wakati wa kazi.
Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi
sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa
kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya
ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika
mazingira ya kutatanisha.
Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza
na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa
watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za
mitaa.
Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa
vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo
mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na
wapiga debe.
Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho
nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi
hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria
zitachukuliwa.
“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha
na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini
huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi
wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa
huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake
umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”
Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji
sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala
yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha
ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho
za vikao.
Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa
Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro,
walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi
kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.