Recent Posts

PropellerAds

Friday, April 29, 2016

Iran yaitaka Marekani kuachilia mali

MarekaniIran imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuihimiza Marekani, kuachilia mali yake yaliyoshikiliwa katika benki za Marekani, sambamba na makubaliano ya mwaka uliopita ya vikiwazo wa kinyuklia.
Iran imeghadhabishwa na uamuzi wa mahakama ya juu nchini Marekani kuwa mali yake yote, yenye thamani ya dola bilioni mbili, iliyoshikiliwa nchini Marekani, ni lazima ikabidhiwe jamaa za watu waliouwawa na makundi yanayohusishwa na Tehran.