Kumekuwa na maandamano ya hasira
yaliofanywa na mamia ya watu mjini Cairo baada ya maafisa wa polisi
kumpiga risasi na kumuua mchuuzi mmoja kuhusu kile walioshuhudia
wanasema ni bei ya kikombe kimoja cha chai.
Mtu mmoja zaidi alipigwa risasi na kujeruhiwa katika kisa hicho kilichofanyika mashariki mwa makaazi ya mji mkuu wa taifa hilo.Afisa mmoja mwanadamizi katika kikosi cha polisi amesema kuwa mgogoro huo ulikuwa ni kuhusu bei ya kikombe cha chai.
Kanda za video zimechapishwa mtandaoni zikionyesha uma wa watu ukivunja gari moja la maafisa wa polisi huku ukisema kuwa ''polisi na majambazi''.
Kumekuwa na msururu wa madai ya ukatili unaodaiwa kutekelezwa na polisi katika miezi ya hivi karibuni ambao umesababisha maandamano ya hasira.