Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 30, 2016

Ada ya kupiga simu Ulaya yashuka kwa 75%

Ada ya kupiga simu kupitia mitandao mingine katika
muungano wa bara Ulaya imeshuka kwa kiwango
kikubwa, ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya ada hiyo
kuondolewa kabisa kwa raia wa bara Ulaya mwaka
ujao.
Ada hiyo huwa haiwapendezi raia wengi wa bara hilo
wanaosafiri kwa shughuli za kibiashara na burudani.
Tume ya muungano huo inasema ada hiyo imeshuka
kwa asilimia 75.
Serikali imesema kuwa wale wanaopiga simu ,kupakua
data ama kutuma ujumbe watahifadhi mamilioni ya
pauni kwa ada kufuatia mabadiliko hayo.
Mamilioni ya Waingereza hutumia pauni milioni 350 kila
mwaka kutokana na ada hizo za kupiga simu miongoni
mwa mataifa ya bara hilo,alisema waziri wa uchumi wa
kidijitali Ed Vaizey.