Mwanasiasa anayeheshimiwa wa chama tawala cha
Afrika Kusini ANC , Ahmed Kathrada, amejumuika na
watu wanaoengezeka, ambao wametoa wito kwa Rais
Jacob Zuma ajiuzulu.
Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa
rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya
mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kutengeneza nyumba
yake binafsi.
Bwana Kathrada, ambaye alifungwa kwa miaka mingi
katika kisiwa cha Robben, pamoja na Nelson Mandela,
alisema, Rais Zuma atazidisha watu kukosa imani na
serikali ya Afrika Kusini, ikiwa atabaki madarakani,.
Rais Zuma amesema wazi kuwa hana azma ya kujiuzulu.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 9, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam January 9,
2025,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma za Mag...
34 minutes ago