Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimesema
hakimtambui Dkt Mohamed Ali Shein aliyetangazwa
kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika mwezi
uliopita.
Viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF),
wakizungumza kwa mara ya kwanza tangu kufanyika kwa
uchaguzi huo ambao chama hicho kilisusia, wamesema
hawamtambui Dkt Shein kama rais wa visiwa hivyo.
“Tangu mapema, tangu Jecha (Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha) alipofuta
uchaguzi, tulisema waziwazi kwamba haikuwa halalali.
Walipoitisha uchaguzi wa marudio, tulisema waziwazi
uchaguzi huo sisi hatuutambui na tukawataka wananchi
wasipige kura,” amesema Katibu Mkuu wa CUF Maalim
Seif Sharif Hamad.
Bw Hamad alikuwa mgombea urais wa chama hicho
katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka
jana na ambao matokeo yake yalifutwa na tume.
“Kama Rais ametokana na mchakato ambao
hamkuutambua nyinyi tangu mwanzo, sasa leo kuja
kusema hatumtambui kwa nini iwe ni haramu?
Hatumtambui.”
Chama hicho kimesema kitatumia njia za kidemkrasia
kulalamika dhidi ya Dkt Shein na serikali yake.
Tanzania yasikitika kunyimwa pesa za MCC
Mabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar
Aidha, kimeiomba jamii ya kimataifa kuwawekea vikwazo
watu binafsi waliofanikisha uchaguzi huo wa marudio
ambao chama hicho kimesema ulikuwa “uongozi
haramu”.
Wiki iliyopita, Shirika la Changamoto za Milenia la
Marekani (MCC) lilisitisha ufadhili wa $472milioni
kwa Tanzania likilalamikia uchaguzi visiwani Zanzibar na
utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.
Pesa hizo zilikuwa za kutumiwa katika miradi ya
kusambaza umeme.
Simba SC kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation wamerejesha kwa Jamii
kabla ya mchezo wao na Bravos
-
Kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika
wa Simba SC dhidi ya Bravos ya Angola utakaochezwa Novemba 27, Simba SC kwa
k...
13 hours ago