Recent Posts

PropellerAds

Wednesday, April 27, 2016

Polisi wanasa saa ya dola milioni moja Nigeria

Polisi wa kupambana na ufisadi nchini Nigeria, wamenasa saa ya thamani ya takriban dola milioni moja kutoka kwa nyumba ya waziri wa zamani wa mafuta anayechunguzwa kwa ufisadi.
Saa hiyo ya kipekee ni moja tu kati ya makumi ya mapambo ya dhahabu almasi na fedha zilizonaswa katika operesheni hiyo ya kuvizia katika nyumba ya aliyekuwa waziri wa mafuta wa Nigeria katika utawala uliopita bi Diezani Madueke.

Shirika la kupambana dhidi ya ufisadi la Nigeria (Economic and Financial Crimes Commission) limeithibitishia BBC kuwa bi Madueke anachunguzwa kufuatia madai ya ufisadi.
Mabilioni ye fedha zilitoweka katika wizara hiyo akiwa mamlakani.
 
Fedha hizo zilikuwa sehemu ya mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta katika soko la kimataifa.
Mwaka uliopita bi Madueke alikamatwa na kuhojiwa na maafisa wa upelelezi wa Uingereza lakini akaachiwa kwa dhamana.
 
Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alichaguliwa kwa nia ya kumaliza kabisa ufisadi uliokuwa umekithiri nchini humo.
Rais Muhammadu ameahidi kutokomeza kabisa ufisadi.