Recent Posts

PropellerAds

Saturday, April 16, 2016

Wanajeshi wa Amisom waua watu wanne Somalia

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini
Somalia (Amisom) wamewaua watu wanne viungani
mwa mji wa Bulla Marer kusini mwa Somalia, wakazi
wa eneo hilo wanasema.
Waliouawa ni pamoja na mwanamke mkongwe na mtoto
wa umri wa miaka tisa.
Wakazi wa mji huo ulioko jimbo la Lower Shabelle
wameandamana mjini kushutumu mauaji hayo.
Kwa mujibu wa wakazi, wanajeshi waliouawa walikuwa
kwenye gari ndogo waliposimamishwa na wanajeshi wa
Amisom, kuamriwa watoke nje na kisha wakapigwa
risasi.
Abdiwahid Maalim Ibrahim, ambaye ni mwanawe ajuza
aliyeuawa na babake msichana aliyeuawa, ameambia
idhaa ya Kisomali ya BBC kwamba watu hao waliouawa
walikuwa wakielekea Mogadishu kutafuta matibabu.
Wanajeshi wa AU wanafanikiwa Somalia?
“Mapema leo, mamangu aliyekuwa na umri wa miaka
80 na binti yangu wa miaka tisa walikuwa wakiugua na
waliondoka Bulla Marer wakitumia gari lililokuwa
likiendeshwa na marafiki zangu wawili kuelekea
Mogadishu,” amesema Ibrahim.
"Wanajeshi wa Amisom waliwasimamisha viungani mwa
mji na kuwaua wote.”
Kikosi cha Amisom kimethibitisha kwamba kuna watu
wanne waliouawa lakini kikasema hawakuuawa makusudi.
Msemaji wa Amisom Kanali Joe Kibet, ameambia BBC
Somali kwamba dereva wa gari hilo alikaidi agizo la
kusimama.
Tarehe 31 Julai, 2015 wanajeshi wa Amisom waliauwa
raia kadha harusini katika mji wa Marka , kusini mwa
Somalia kisa kilichoshutumiwa vikali.