Recent Posts

PropellerAds

Thursday, April 28, 2016

Mtoto wa miaka 2 amuua mamake Marekani

Price
Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.
Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.
Mwanamke huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake Andre Price amesema.
Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi.
Mamake Price na mwanawe mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walikuwa kwenye gari hilo wakati wa kutokea kwa kisa hicho.
Bw Price alisema ana binti mwingine mkubwa, lakini akasema Patrice alikuwa na bidii sana.
“Sasa hayupo nasi tena. Inaniuma sana,” Bw Price aliambia kituo cha habari cha WISN, Milwaukee.
Mwezi uliopita, mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt katika jimbo la Florida katika hali sawa.
Bi Gilt alinusurika na majeraha.

Related Posts:

  • Miili ya wahamiaji yapatikana:Libya Taarifa kutoka Libya zinasema kuwa miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji, imepatikana ikiwa imetapakaa katika mwambao wa bahari karibu na mji wa Zuwara. Baadhi ya taarifa zinasema zaidi ya miili 85 imeonekana ikiwa… Read More
  • India yaanzisha huduma ya kusambaza maji matakatifu Serikali ya India imesema kuwa inajiandaa kuzindua huduma za kusambaza maji matakatifu na chakula kupitia ujumbe. Waziri anayesimamia huduma ya kutuma ujumbe ya posta Ravi Shankar Prasad amesema kuwa maji kutoka kwa maeneo… Read More
  • Rais wa Angola amteua bintiye mkuu wa mafutaRais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, amemteua binti yake ambaye ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika kuwa mkuu wa shirika la mafuta la kitaifa la Sonagol. … Read More
  • Dawa zilimuua Prince:Madaktari Uchunguzi wa kidaktari kutoka jimbo la Minnesota nchini Marekani umebaini kuwa mwanamuziki Prince alikufa kutokana na kuzidisha kiwango cha dawa. Kwa mujibu wa madaktari waliofanya uchunguzi huo wa kifo cha mwanamuziki… Read More
  • Wataka sheria ya talaka kufutwa India Wanaume na wanawake 50,000 wamesaini azimio la kushinikiza serikali ya India kufutilia mbali sheria ya kutumia neno Talaq, mara tatu kwa misingi ya kuvunja ndoa. Kwa sasa wanaume Waislamu wanaweza kuwataliki wake zao kwa… Read More