Kiongozi wa chama cha Conservative cha Ujerumani
Andreas Scheuer amependekeza kuwa kijerumani kitumike
wakati wa salah misikitini nchini humo badala ya
Kiarabu.
Mwanasiasa huyo aidha anasema kuwa ni sharti
Ujerumani izuie ufadhili wa misikiti kutoka Saudi Arabia
na Uturuki.
Katibu huyo mkuu wa chama hicho cha CSU ambacho
ni mshirika wa chama kinachoongozwa na Kansela wa
Ujerumani bi Angela Merkel cha CDU analaumu siasa za
kiislamu kwa kuhujumu mtagusano baiana ya Wajerumani
waislamu na wakristo.
Maimamu wanaoendesha swala na misikiti nchini
Ujerumani wanapaswa kujifunzia hukohuko Ukerumani
wala sio Arabuni
Maoni yake yanawadia huku kukiwa na mtafaruk mkubwa
wa kidiplomasia baina ya Ujerumani na Uturuki
kuhusiana na uhuru wa kujieleza.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasilisha
mahakamani kesi dhidi ya mchekeshaji mjerumani Jan
Boehmermann.
Rais huyo anadai kuwa Boehmermann alimkosoa heshima
katika moja ya mashairi yake iliyopeperushwa na
runinga ya taifa ZDF.
Inadaiwa kuwa mchekeshaji huyo nguli aliwatahadharisha
watazamaji kuwa atakachokisema kitakiuka haki za
kujieleza za wajerumani kabla kumtusi rais Erdogan.
Jan alisema kuwa Erdogan hushiriki ngono na wanyama
kama vile mbuzi na kondoo.
Waendesha mashtaka nchini Ujerumani wangali
wanachunguza tukio hilo ilikubaini iwapo msanii huyo
nguli atashtakiwa kwa kumkejeli na kumtusi rais wa
taifa la kigeni.
Serikali ya Uturuki ilisajili kesi hiyo rasmi kw balozi wa
Ujerumani nchini humo mjini Ankara.
Hilo ndilo tukio la pili ambalo linaonekana kuikasirisha
sana Ankara.
Awali wimbo mmoja uliopeperushwa kwenye runinga
inadaiwa kuukejeli uongozi wa bw Erdogan.
Mchekeshaji huyo amepewa ulinzi mkali wa polisi na
hata shoo yake ijayo imepigwa marufuku.
Kesi hiyo imemweka pabaya Kansela wa Ujerumani bi
Merkel kwani yeye pamoja na viongozi wenza wa bara
Ulaya wanaisihi Uturuki(Erdogan) kutekeleza upande
wao wa makubaliano ya kusitisha wimbi la wahamiaji
kutoka Syria.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 10, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 10,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
9 hours ago